October 12, 2017

YANGA KUIVAA KAGERA SUGAR UWANJA WA KAITABA ‘BILA NYOTA WANNE’

IMG_0276-640x427
Mabingwa watetezi  Yanga tayari wametua salama kwa ndege mjini Bukoba mkoani Kagera kwa vita ya kusaka alama tatu dhidi ya wenyeji timu ya Kagera Sugar Mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara utakaochezwa siku ya Jumamosi Oktoba 14 kwenye uwanja bora kabisa wa Kaitaba.
Katika mchezo huo, Yanga itawakosa wachezaji wake Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao wanasumbuliwa na majeraha Wachezaji wengine watakaokosena ni Ramadhani Kabwili na Said Musa ambao wapo kwenye timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambayo ipo kambini ikiendelea na mazoezi.
Kwa mujibu wa afisa habari wa Yanga Dismas Ten, Ngoma hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Kagera Sugar lakini anaweza akatumika kwenye mchezo dhidi ya Stand United kwa hiyo atasafiri na timu kuelekea Kanda ya Ziwa.
Yanga waingia katika dimba la Kaitaba wakiwa na kumbukumbu ya kushinda magoli 6-2 msimu uliopita wakiwa chini ya Mtaalamu Hans Van Der Pluijm ambaye kwa sasa yupo Singida United huku wakianza kwa kusuasua msimu huu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE