October 16, 2017

WEAH KUCHUANA NA BOAKAI DURU YA PILI YA UCHAGUZI

Tume ya uchaguzi nchini Liberia imetangaza kuwa aliyekuwa mwanasoka maarufu wa kimataifa George Weah na makamu wa Rais wa Liberia Joseph Boakai Watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.
Tume ya uchaguzi nchini Liberia imetangaza kuwa aliyekuwa mwanasoka maarufu wa kimataifa George Weah na makamu wa Rais wa Liberia Joseph Boakai Watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais inayotarajiwa tarehe 7 Novemba. Weah alipata asilimia 39 ya kura huku Boakai akipata asilimia 29.1 katika duru ya kwana ya uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki iliyopita, hivyo hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kuepusha duru ya pili ya uchaguzi.
Atakayeshinda duru ijayo atamrithi Rais Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza barani Afrika kuwa Rais anayesataafu baada ya kuwa madarakani kwa miaka 12. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jerome Korkoy amesema idadi ya wapiga kura iliyojitokeza kushiriki katika uchaguzi ilikuwa ni asilimi 74. Wapiga kura wana chaguo kati ya Boakai ambaye amehudumu katika nyadhifa mbali mbali serikalini kwa zaidi ya miongo mitatu au Weah ambaye ni maarufu mno licha ya kutokuwa na uzoefu  katika ulingo wa kisiasa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE