October 18, 2017

TANZANIA YATAMBA KUFANYA VYEMA MISS WORLD

mis 1
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt . Kulia Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na kushoto ni  Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
mis 2
Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy  (kushoto) akimkabidhi bendera Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete (katikati)  katika hafla ya kumuaga iliyofanyika jana kwenye hotel ya Hyatt . Kulia Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
mis 3
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete akiwa katika pozi mara baada ya kukabidhiwa bendera kwenye halfa fupi iliyofanyika kwenye hotel ya Hyatt
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Miss World Tanzania, Julitha Kabete (21) ametamba kufanya vyema katika mashindano ya 67 ya kumsaka mrembo ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Sanya, nchini China mwezi ujao.
Julitha ambaye anaondoka leo, amesema kuwa amejiandaa vyema ili kuiletea sifa Tanzania katika mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Novemba 18 kwenye ukumbi wa Sanya City Arena in Sanya, China PR.
 Stephanie na kushirikisha jumla ya warembo 120. Julitha anaondoka leo kwenda China chini ya udhamini wa Turkish Airline. Mrembo huyo aliagwa na kukabidhiwa bendera na  Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
“Nimejiandaa vizuri katika mashindano haya, nina uzoefu mkubwa kwani nilishinda mashindano ya Miss Dar City Center, Miss Ilala na kwenye fainali za miss Tanzania 2016 ambako niliingia tano bora. Pia nilishiriki mashindano ya Afrika na kufanya vyema,” alisema Julitha.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema Julitha ni mrembo wa 23 kuiwakilisha nchi kwenye Miss World.
“Mwaka huu shindano la Miss Tanzania limechelewa kufanyika, hivyo tukaamua kumtea Julitha akatuwakilishe kwenye Miss World, uteuzi wake umezingatia vigezo vyote na hakuna shaka atafanya vizuri katika fainali hizo ambazo tumekuwa na rekodi ya kutwaa taji la Miss World Afrika na mataji mengine,” alisema Lundenga.
Mrembo huyo aliondoka nchini jana usiku kuelekea katika kambi ya Miss World nchini China ambapo atachuana na warembo wengine kutoka mataifa zaidi ya 120 kusaka mshindi katika fainali itakayofanyika baadae Novemba nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE