SHIRIKA
la Taifa la Madini (Stamico) limepata mtambo wa uchorongaji kwa kutumia
upepo (Air Rotary Drill Rig) wenye thamani dola za Kimarekani milioni
1.3 utakaotumika kupata taarifa za kijiolojia na mashapo kwa wachimbaji
wadogo .
Kunufaika kwa wachimbaji wadogo kunatokana na stamico kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa
Stamico, Elexender Muganda amesema kuwa mtambo umetengenezwa nchini
Canada ambapo mtambo huo utasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za
kijiolojia na mashapo katika maeneo yao kwa gharama nafuu.
Amesema
mtambo huo umetolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini chiini ya
ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa usimamizi endelevu wa
rasilimali ya madini Tanzania (SMMRP).
Muganda
amesema huo una uwezo wa kuchoronga miamba kwa kutumia upepo na kwa
haraka zaidi kati ya kina mita 30 hadi 200 na kwa gharama ambazo
mchimbaji mdogo anamudu na kuachana uchimbaji wa kubahatisha pamoja
kuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha.
Aidha
amesema kuwa wachimbaji wadogo wanaohitaji huduma za uchorongaji kwa
kutumia upepo wafike katika ofisi za Stamico ili kupata taarifa zaidi.
Mwenyekiti
wa Bodi wa Stamico, Elexender Muganda akizungumza na waandishi habari
juu shirika la Taifa la Madini (Stamico) kupata mtambo wa kisasa wa
uchorongaji kwa kutumia upepo , jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela
akitoa ufafanuzi juu ya mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba jijini
Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano, Koleta Njelekela.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji, Alex Rutagwelela akiangalia
mtambo wa uchorongaji wa miamba Bandarini, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa mtambo wa uchorongaji.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE