October 31, 2017

SPIKA NDUGAI MGENI RASMI KATIKA UFUNGUZI WA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 90 YA KANISA KUU LA ROHO MTAKATIFU, DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA

IMGL0055
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katika) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa kuu la Roho Mtakatifu Mjini Dodoma. wa tatu kulia ni Askofu wa Dayosisi hiyo, Dkt. Dickson Chilongani. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonesho hayo.
IMGL0567
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na waumini wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa hilo Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonyesho hayo.
5Y2A2866
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mheshimiwa Albert Obama akiongoza kikao cha pamoja kati ya kamati hiyo na watendaji kutoka kituo cha zana za kilimo na Teknolojia Vijijini (KAMATEC) wakati wakipokea, kujadili na kuchambua taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa KAMATEC kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
IMGL9926
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, katika kikao cha kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kushoto ni kiongozi wa msafara na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, Mheshimiwa Dkt. Mark Yeboah na wanne kulia ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai
IMGL9946
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza kiongozi wa msafara na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, Mheshimiwa Dkt. Mark Yeboah (wa pili kushoto) wakati wa kikao na  wajumbe wa kamati ya fedha kutoka Bunge la Ghana, kikilenga kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kulia ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai
IMGL0142
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipatiwa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa kanisa kuu la Roho Mtakatifu, Dayosisi ya Central Tanganyika, Ndg. Grace Lisasi (katikati) alipotembelea Banda la Umoja wa Wanawake wa Kikristo (UWAKI) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 90 ya Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya kanisa hilo Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, alikuwa mgeni rasmi katika Maonesho hayo.
PICHA NA OFISI YA BUNGE

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE