October 13, 2017

SHEKH PONDA AJISALIMISHA POLISI

Sheikh Ponda wa Tanzania

Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa maeneo maalum mjini Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.
Kiongozi huyo wa dini aliwasili katika kituo hicho cha polisi siku ya Ijumaa akiwa na wakili wake Abdallah Safari.
Bwana Mambosasa siku ya Alhamisi alimwagiza Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyotoa.
Kulingana na kamanda huyo , Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo akamatwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE