October 1, 2017

RIPOTI YA LEMA NA NASSARI KUHUSU RUSHWA KWA MADIWANI


Dar es Salaam. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kesho Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.
Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.
Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.
Lema akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE