October 13, 2017

RC MASENZA AAGIZA NYUMBA ZISIZO NA VYOO BORA ZIPANDISHWE BENDERA NYEKUNDU

RC iringa Amina Masenza katikati Akita akigizo kwa viongozi Kilolo 
Mkurugenzi kilolo kulia akisalimiana na RC masenza 
Mkuu wa mkoa Iringa na wataalam Wakikagua vyoo vya shule ya Msingi Pomerin

Mkuu wa mkoa akikagua choo cha mwananchi wa kawaida 
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ameagiza halmashauli ya wilaya ya Kilolo kuanza utaratibu wa kupandisha bendera nyekundu kwa nyumba zote zisizo na vyoo bora. 

Agizo hilo alitoa jana wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa vyoo bora katika shule za msingi,ofisi za umma na makazi ya wananchi kwenye kata ya Ng'uruwe wilayani Kilolo .

Alisema kuwa kasi ya ujenzi wa Nyumba inapaswa kuendana na kasi ya ujenzi wa vyoo bora na kuwa hatavumilia kuona Nyumba isiyo na choo bora.

"sitavumilia kuona nyumba isiyo na choo bora ndani ya wilaya ya kilolo na mkoa mzima wa Iringa kule wilaya ya Iringa hasa Pawaga ambako kuna kipindupindu wamekuwa na utaratibu wa kupandisha bendera nyekundu nyumba zisizo na vyoo bora kwa muda na baada ya hapa muda kujenga choo bora ukiisha unafikishwa mahakamani "

Mkuu huyo wa mkoa alisema ni vema kila halmashauri kuwe na mashindano ya usafi kwa ngazi ya kijiji, kata na wilaya kwa wilaya ila pia kuendelea kuwafikisha mahakamani wote watakao shindwa kuwa na vyoo bora.

Katika hatua nyingine Masenza alitaka wananchi kuwa makini na matumizi ya maji ya mto Ruaha kwani maji hayo yamepimwa na kukutwa na vimelea vya vidudu vya kipindupindu.

Mkoa wa Iringa una jumla ya asilimia 1.7 ya Nyumba zisizo na vyoo bora.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE