October 31, 2017

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

IMG-20171031-WA0041
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* leo amekabidhi *Mabasi 10 chakavu* ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya *DAR COACH LTD* kwaajili *kufufuliwa upya* na kuwa ya kisasa.
*Mabasi hayo 10* chakavu yanatoka kwenye *Vyombo vya Ulinzi na Usalama* ikiwemo *Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3* ambapo yote kwa pamoja *Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.*
*RC MAKONDA* amesema kuwa Gari hizo *zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90* ambapo ameipongeza Kampuni ya *DAR COACH LTD* kwa kujitolea kukarabati Magari hayo *bila kutumia pesa ya Serikali.*
Aidha *MAKONDA* amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo *Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya* pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.
*RC MAKONDA* amesema mpango wake wa kuendelea *kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma* kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na *Askari wajivunie kufanyakazi chini ya RC MAKONDA*.
Amemuagiza *Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa* kuhakikisha Ving’ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na *kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa* ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.
Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Sasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo *Kamanda wa Polisi Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAJAB MWENYUMBU, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. NOEL JAMES* ambapo wote kwa pamoja wamempongeza *RC MAKONDA.*
IMG-20171031-WA0043
IMG-20171031-WA0044 IMG-20171031-WA0045 IMG-20171031-WA0047 IMG-20171031-WA0048

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE