October 30, 2017

RAIS WA TFF-SOKA LINAHITAJI WATAALAMU WA KUTOSHA NCHINI


Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia ,amesema ili soka la Tanzania iweze kusonga mbele lazima kuwe na wataalamu watakaoweza kutafsiri sheria mbalimbali za mchezo huo unaopendwa na wengi nchini.

Aidha ameupongeza mkoa wa Pwani kwa kuandaa mafunzo mengi ya waamuzi na makocha hivyo kuwa moja ya mikoa yenye wataalamu wa soka.

Karia aliyasema hayo wakati wa fainali ya michuano ya Kabumbu Mazingira Cup iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Msata,ambayo yaliandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga.

Alieleza COREFA kwa kushirikiana na wadau wake imeweza kuandaa mafunzo ya walimu wa soka (wataalamu)na waamuzi hali ambayo itasaidia kuinua mchezo wa soka hasa mikoani.

“Mikoa ya Pwani na Morogoro imejitahidi sana katika kuzalisha wataalamu hao jambo ambalo linatakiwa lifanywe na kuigwa na mikoa mingine”alifafanua Karia.

“Kila mkoa unapaswa kuzalisha wataalamu wa kutosha kwa kutoa mafunzo kwa wadau wanaopenda fani hizo kwani kukiwa na wataalamu wengi soka letu litaweza kukua,” alisema Karia.

Nae mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alisema lengo la kuwa na michezo kama hiyo ni kuendeleza vipaji vilivyopo pembezoni.

Alieleza kwamba,katika mashindano hayo kumeonekana vipaji vingi ambavyo vikiendelezwa Tanzania itakuwa na hazina kubwa ya wachezaji.

Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Pwani COREFA Hassan Hassanoo ,alisema kuwa mkoa huo utaendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wa soka ili kukuza mchezo huo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga alisema aliandaa mashindano hayo kwa majimbo mawili ya Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kuhamasisha masuala ya usafi kwa Wanabagamoyo.

Mwanga alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa yanakwenda pamoja na jumbe mbalimbali za usafi pamoja na utunzaji mazingira bila kusahau ushiriki wa jamii katika michezo.
Katika fainail hiyo timu ya soka ya kata ya Pera,imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Kabumbu Mazingira Cup na kufanikiwa kutwaa bajaj.

Pera walifanikiwa kuifunga timu ya soka ya Kata ya Bwilingu waliojinyakulia pikipiki ya matairi mawili kwa 1-0 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Msata.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyoya,yalihusisha timu za kata zote za Halmashauri ya Chalinze.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE