October 24, 2017

NI STARS NA BENINI,NOVEMBA 11 MWAKA HUU


Kocha  wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewarejesha kikosini kiungo Farid Mussa na mshambuliaji, Elias Maguri kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.
Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu.
 Mayanga leo ametaja wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.  
Katika kuwaita wachezaji hao amewaorodhesha Maguri aliyekuwa anacheza Oman na Farid Mussa anayecheza Tenerife B ya Hispania, ambao wote hakuwaita kwenye mchezo uliopita dhidi ya Malawi, uliomalizika kwa sare ya 1-1 Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili(Yanga)
Mabeki :Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
Viungo :Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadida/Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) 
Washambuliaji: Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).  

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE