October 4, 2017

MWENYE UALBINO AKATWA MKONO

Mzee Nassoro Msingili (75) mwenye ualbino mkazi wa Kijiji cha Nyarutanga wilayani Morogoro amekatwa mkono wa kushoto na watu wasiojulikana na kutoweka nao kusikojulikana.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leons Rwegasira akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za polisi mkoani hapa leo Jumatano amesema tukio hilo lilitokea juzi saa 6 usiku huko kijiji cha Nyarutanga.

Rwegasira amesema mzee Msingili akiwa nyumbani kwake amelala alivamiwa na watu wasiojulikana na kisha kumkata mkono wake wa kushoto na kukimbia nao kusikojulikana.
Amesema majeruhi huyo kwa sasa amelazwa katika Kituo cha Afya Dutumi na kwamba anaendelea kupatiwa matibabu na afya yake inaendelea kuimarika.
Kaimu Kamanda huyo amesema jeshi hilo kwa sasa linaendelea kuwasaka watu hao wasiojulikana na kwamba wanapinga vikali mauaji na ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi huku akiwataka wananchi kutoa ushirikikano.
Mbali na hilo pia amezungumzia kushikiliwa kwa watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Ofisa Tarafa wa  Lupilo, Beno Polisi.
Rwegasira amesema watu hao wanashikiliwa na wengine zaidi wanasakwa kuhusiana na mauaji ya ofisa huyo wilayani Ulanga aliyeuawa kikatili kwa kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa shoka na watu wasiojulikana.
Rwegasira amesema bado upelelezi wa mauaji hayo ya kikatili unaendelea kufanywa na jeshi hilo la polisi na kulaani vikali vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji na ukatili kwa wengine.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE