October 29, 2017

MISS UNIVERSE TANZANIA 2017 NI LILIAN MARAURE

1
 Miss Universe Tanzania 2016, Jihan Dimachk (kulia) akimvisha taji mshindi mpya wa shindano hilo mwaka huu  Lilian Erica Maraure mara baada ya kutwaa taji hilo jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Posta jijini.
2
Miss Universe Tanzania 2017, Lilian Erica Maraure akiwa katika pozi  pozi mara baada ya  kutwaa taji hilo jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Posta jijini.
3
Miss Universe Tanzania 2017, Lilian Erica Maraure (katikati) akipozi katika picha pamoja na mshindi wa pili Anitha Mlay (kushoto) na mshindi wa tatu  Melody Tryphone mara baada ya kutangazwa kushinda katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wa jijini.
4
Majaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania wakifuatilia kwa umakini shindano hilo.
5
Jaji Mkuu, wa Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi akitangaza warembo watano bora walioingia katika mashindano hayo.
6
Kwa raha zao! Jaji Mkuu, wa Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi kushoto na Miss Universe Tanzania wa mwaka jana, Jihan Jihan Dimachk wakiwa katika ‘red carpet’.
………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Lilian Erica ametwaa taji la Miss Universe Tanzania katika mashindano yaliyofnyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Lilian ambaye ni mtangzaji za TBC International ameshinda taji la 10 la mashindano hayo yalioanza kufanyika nchini mwaka 2007 ambapo mrembo Flaviana Matata alishinda taji hilo na baadaye kumaliza ndani ya 10 bora katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico..
Mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo wengine hasa mshindi wa pili Anitha Mlay na mshindi wa tatu  Melody Tryphone. Warembo Rogathe Ally na Glory Gideon nao walimaliza katika nafasi ya nne na ya tano. Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications chini ya mkurugenzi, Maria Tsehai Sarungi.
Liliani alivishwa taji na Miss Universe Tanzania wa mwaka jana,  Jihan Dimachk. Warembo wengine walioshiriki katika mashindano hayo ni Silvia Mkomwa, Prisca Dastan(wote kutoka Dar es Salaam) ambapo kutoka Mwnza ni Maureen Foster na Mary Peter na kutoka Mbeya alikuwa Zahra Abdul.
Warembo hao waliweza kutoka burudani ya aina yake chini ya mkufunzi, Lilian Loth ambaye alimaliza nafasi ya pili katika mashindano ya mwaka jana na pia ni mshindi wa pili wa shindano la Miss Africa second princess.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana, Bonuzi  na burudani safi ilitoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), na Jeff Mduma ambaye aliimba wimbo wa “A beautiful”.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE