October 18, 2017

MGOMBEA UBUNGE WA CUF AHAMIA ACT-WAZALENDO

Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini katika Uchaguzi wa mwaka 2015 kupitia chama cha CUF, Kindamba Namria amehamia ACT-Wazalendo kwa madai ya kutoridhishwa na muenendo wa CUF kufuatia mgogoro ulipo baina ya viongozi wa ngazi za juu kwenye chama hicho.
Wakati akizungumza baada ya kutambulishwa rasmi na Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, Namria amesema kwa sasa CUF imejikita katika majibizano badala ya kutetea wananchi, kitendo kilichopelekea kukihama chama hicho.
“Naamini kwenye masuala, na ndiyo sababu nimehama CUF kwa sababu kuna majibishano ambayo hayana tija kwa watanzania. Mtu unajitambulisha Mimi ni CUF fulani, mnatumia miaka 4 kupambana na uhalali wenu kisha mje mtetee wananchi, nimeona kubaki kwenye chama hicho si salama kwangu,” amesema.
Namria amesema kwa sasa CUF ilitakiwa kuibua masuala yenye tija kwa ajili ya kutetea wananchi, haki za kiraia na kidemokrasia badala ya kugombania uhalali wa uongozi wa chama.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE