October 26, 2017

MEYA MANISPAA YA IRINGA ATAKA USIMAMIZI MZURI WA BARABARANa: Sima Bingileki- Afisa Habari Manispaa ya Iringa.

Wananchi wa Kata ya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa wametakiwa kuwa walinzi na watumiaji wazuri wa barabara ya lami ya Don Bosco-Mawelewele inayojengwa kwa kiwango cha lami nzito chini ya ufadhili wa benki ya Dunia kwani kuwepo kwa barabara  katika eneo hilo kutachochea maendeleo na kuleta tija kwa watumiaji na wakazi  hususan katika eneo hilo.

Barabara hiyo ya lami nzito itagharimu jumla ya shilingi bilioni 3,574,401,000.00/= mpaka kukamilika kwake ambapo inatarajiwa kukamilia utengenezaji wake tarehe 14/11/2017 chini ya mkandarasi Southern Link Limited.

Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Fedha na Uongozi inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe amesema ni jambo la kujivunia kwa manispaa ia Iringa kuwa Miongoni mwa Halmashauri 18 za Miji na Manispaa za Tanzania zilizo katika utekelezaji wa Mpango wa Uimarishaji Halmashauri za Miji ( Urban Local Government Strenghthening Programme –ULGSP). 

Amesema wananchi wa Kata ya Mkwawa wanatakiwa kuwa na matumizi sahihi ya barabara hiyo na kutunza mifereji kwani kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa barabara hivyo kurudisha nyuma maendeleo na tija kwa wakazi wa eneo hilo na wakazi wote wa Manispaa ya Iringa. Amewaasa kutunza mifereji ya maji inayopita pembezoni mwa barabara hiyo na kutotumia mifereji hiyo kwa matumizi yasiyo husika ikiwemo kumwaga maji taka katika mirereji.
Mpaka sasa mradi huu wa barabara umetumia jumla ya shilingi bilioni 1,604,543,818.04/= ambapo mpaka kukamilika kwake utakuwa umegharimu jumla ya shilingi bilioni 3,574,401,000.00/=  Mradi huu wa barabara ya DonBosco Mawelewele unajengwa kwa kutumi fedha za ufadhili wa benki ya Dunia

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE