October 17, 2017

MBOWE KUFANYA MKUTANO NA WANAHABARI LEO KUHUSU LISSU


 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kesho Jumanne Oktoba 17, 2017 atazungumzia maendeleo ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7, amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, baada ya kuulizwa kuhusu hali ya Lissu, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema:
“Kesho saa 5:00 asubuhi nitakuwa na mkutano na waandishi wa habari, nitazungumzia hali ya Lissu na mambo mengine yanayoendelea.”
Baadaye katika taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene amesema mkutano huo utafanyika makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kupitia Mwenyekiti, Freeman Mbowe chama kitatoa taarifa kwa Taifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango, gharama za matibabu,” amesema Makene.
#Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE