October 30, 2017

MAMENEJA TEMESA WAPEWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MANUNUZI NA MIKATABA


PIC 1
Mhandisi Dkt. Ramadhan S. Mlinga kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET) akitoa ufafanuzi wakati  akitoa mafunzo kwa Mameneja wa Mikoa na Vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Mafunzo hayo yanayohusu Usimamizi wa Manunuzi na Mikataba yameanza leo na yanafanyika  katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia Chuo kikuu cha Dar es Salaam (COET).
PIC 2
Baadhi ya Mameneja wa Mikoa, vituo na Idara mbali mbali  kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiendelea na mafunzo yanayohusu Usimamizi wa Manunuzi na Mikataba yanayotolewa katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET). Mafunzo hayo yamelenga kuwapatia uwezo wa kusimamia Mikataba pamoja na Manunuzi mameneja hao na yatafanyika kwa siku tano chuoni hapo.
PIC 3
Baadhi ya Mameneja wa Mikoa, vituo na Idara mbali mbali  kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza mkufunzi  Mhandisi Dkt. Ramadhan S. Mlinga (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiwapa mafunzo kuhusu Usimamizi wa Manunuzi na Mikataba. Mafunzo hayo yanafanyika katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia Chuo kikuu cha Dar es Salaam (COET) na yanatarajiwa kumalizika baada ya siku tano.
PIC 4
Mameneja wa Mikoa, vituo na Idara mbali mbali kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkufunzi Mhandisi Dkt. Ramadhan S. Mlinga (katikati). Mameneja hao wanahudhuria Mafunzo ambayo yanafanyika katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET) na yamelenga kuwajengea uwezo katika masuala ya Usimamizi wa Manunuzi pamoja na Mikataba.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE