October 29, 2017

MAFAMASIA MAFAMASIA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU, DKT. ROBERT SALIM
PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA

Wafamasia na wafanyabiashara wenye maduka binfasi ya dawa za binadamu na mifigo wameombwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uuzaji dawa.

Hayo yalisemwa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Robert Salim katika maadhimisho ya ‘Siku ya Famasi’ yaliyoandaliwa na chama cha wanafanzi wa famasi –Tanzania (TAPSA), tawi la Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU) kwa ufadhili wa shirika la Austrian Leprosy Relief Association kwa kushirikiana shirika la Action Medeor.

Maadhimisho hayo ambayo yalienda sambamba na kaulimbiu isemayo, ‘MAPAMBANO DHIDI YA USUGU WA DAWA NI YA KILA MMOJA WETU.’ 

Dkt. Salim alisema kuwa wafamasia na wafanyabiashara wanatakiwa kuuza dawa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa mfano, kuuza dawa za moto kwa prescription na kutunza dawa vizuri.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ina lengo la kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.

Mganga mkuu huyo aliviomba vyuo vyote nchini vya famasi viwaandae vijana kufungua viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa vile malighafi nyingi zipo hapa Tanzania.

“Kuna mistu, pamba, gypsum na kadhalika ambazo ni hazina kubwa ya dawa za tiba asili,” alisema Dk. Salim.

Pia, aliwataka wanafunzi wanaosomea masomo ya famasia wa kimaliza masomo yao waanzishe viwanda vidogo vidogo vya dawa, ili kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano ya sera ya viwanda ambapo kutasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijina.

Naye, Mwenyekiti wa TAPSA-RUCU Ndamo Adam alisema kuwa usugu wa dawa ni janga la kifaifa husuani nchi ambazo zipo katiak ukanda jangwa la sahara kusini.

Alisema kampeni ya kupambana na usugu wa dawa ni jukumu la kimoja kwa vile dawa zote zinazotumika kutibu magonjwa ya kuambukiza huweza kuathiriwa na usugu wa dawa. 

Adam alifafanua kuwa usugu wa dawa ni hali ya dawa kushindwa kuua au kuzuia ukuaji wa vimelea vya magonjwa na vimelea vya magonjwa ndivyo hujenga usugu dhidi ya dawa.

“Dawa zinazotumika mara kwa mara kama vile Ampicilin, Ciprofloxacin, Tetracycilin, Erythromycin, Metronidazole, Amoxicilin, Chloramphenicol na Griseofulvin zinaathiriwa zaidi,” alisema Adam.

Alisema kuwa moja ya usugu wa dawa ni kutotumia ‘dozi’ sahihi ya dwa na kwa muda ulioelekezwa pamoja na kutumiaantibayotiki kutibu magonjwa yasiohitaji antibiotiki.

Kwa upande wake, Mfamasia na mwalimu wa Famasia katika chuo kikuu katoliki cha Ruaha (RUCU) Gasper Baltazary alisema kuwa kampeni dhidi usugu wa dawa iwe endelevu.

Alisema kuwa kuna umuhimu mukubwa wa usimamia ugunduzi sahihi wa magonjwa (kwa vipimo), utoaji dawa kwa dozi sahihi (vipimo), muda sahihi, kuzingatia masharti ya daktari pamoja na kutoa dawa ambazo hazijaisha muda wake wa matumizi.

Baltazary alisema kuwa siku ya famasi ni moja kati ya majukumu ya chama cha TAPSA ambapo lengo ni kuwaleta wanafunzi na wataalamu mbalimbali wa kada ya afya ili kujadili viti ambavyo vinahusu afya.

Alisema kuwa ukosefu wa elimu ndio chanzo kikubwa cha uwepo ya usugu wa dawa, hivyo basi jamii na wafanyabiashara waache kutumia dawa bila kufanya vipimo na kuuza dawa kwa lengo la kupata tu pesa.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE