October 19, 2017

KESI YA LULU DHIDI YA MAUAJI YA KANUMBA YAANZA KUSIKILIZWA

 Elizabeth Michael "Lulu" akiwa katika Mahakama kuu Dar es salaam akisubiri akitafakari jambo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukusudia
 Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael "Lulu" akiwa katika Mahakama kuu Dar es salaam akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukusudia. Lulu anakabiliwa na kesi ya kifo cha aliyekuwa muigizaji mwenzake wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012 jijini Dar es salaam. Kulia ni Mama wa Muigizaji huyo.
Shahidi wa Kwanza wa upande wa upande Jamuhuri katika kesi ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya marehemu Steven Kanumba, inayomkabili msanii maarufu nchini, Elizabeth Michael ameieleza mahakama kuu kuwa licha ya kumwambia Lulu abaki na Kanumba yeye alipomfuata daktari lakini aliondoka na kumuacha peke yake

Shahidi huyo, Bosco Seth (30) ambaye pia ni kaka Wa Marehemu Kanumba ameyasema hayo leo mapema mbele ya Jaji Sam Rumanyika wakati akitoa ushahidi wake. Kabla ya kuanza kutolewa kwa ushahidi, Lulu alikumbushiwa mashtaka yake ambapo ilidaiwa April mwak 2012 huko Sinza Vatcan wilaya ya Kinondobi alimuua bila kukusidia Kanumba, Lulu alikana shtaka hilo.

Akiongozwa na Wakili wa serikali Faraja George, Bosco amesema baada baada ya kupata taarifa za kudondoka kwa Kanumba kutoka kwa Lulu alimpigia simu daktari wao aliyemtaja kwa jina la Paplas ambaye alimtaka kwenda kumchukua Hospitalini kwake na kwa kuwa hakukuwa na usafiri aliwasha Gari na kimfuata na kumuomba Lulu abaki na Kanumba.
Wakati narudi na Dk, Lulu alinipigia simu akasema Kanumba nimemuwekea mpaka maji kifuani lakini haamki ninaindoka, nikamwambia nisubiri lakibi mpaka nafika pale sikumkuta*.

Alidai baada ya Dr kufika na kumpima alimshauri wampeleke Muhimbili, ambapo kwa msaada wa jirani yao aliyemtaja kwa jina la Baraka walimbeba Kanumba na kumuingiza kwenye gari hadi Muhimbili.

Amedai wakati wanaangaika kumuingiza Kanumba kwenye gari, mama mwenye nyumba alisikia akafungua mlango aliposikia tatizo nae aliwasha gari lake na kutusindikiza, ambapo walienda moja kwa moja Emergency na baada kumfanyia Kanumba uchunguzi Dr aliwaambia kuwa ameishafariki na kituambia tufuate taratibu za polisi.

Amedai walienda polisi Urafiki ambako wakiwa huko Lulu alikuwa akimpigia Dr Paplas Simu ndipo polisi wakamuomb Dr aweze kuwasaidia kumpata Lulu ambapo asubuhi ya Aprili 7, baada ya wao kumaliza kuhojiwa Lulu alakamatwa.

Akielezea jinsi tukio Lilia to lies alidai, Aprili 4 mwaka 2012 alishinda nyumbani na kaka Kanumba toka asubuhi na ilipofika mida ya saa kumi jioni, Kanumba alimuomba asitoke na wangetoka pamoja usiku wa saa sita.

Akadai ilipofika SAA sits kasoro za usiku Kanumba alimwambia wajiandae watoke, ambapo yeye alikuwa Wa Kwanza kumaliza kujiandaa lakini alipotoka chumbani kwake akielekea sebuleni, alikutana na Kanumba akipita kwenye koridoni huku akiwa amevalia taulo kuelekea sebuleni, akipaka Mafuta kichwabi, sebuleni kwa nje kulikuwa na Gari la Lulu, nikamuuliza mbona tunachelewa akanijibu sasa hivi tunaondoka.

Akadai kuwa, Kanumba ndiye alimfungulia mlango lulu, waliingia wote ndani akiwa chumbani kwake ambako alirudi kumsubiria Kanumba huku mlango wake ukiwa wazi kidogo, wakati wakitembea Koridoni kuelekea chumbani kwa Kanumba alisikia wakigombana huku Kanumba akimuuliza lulu kwa nini anaongea na boyfriend wake mbele yake,.

Aliendelea kudai kuwa muda wote huo walikuwa wakivutana, Lulu akitaka kutoka nje na Kanumba akimvutia ndani mara waliingia chumbani na mlango ukafungwa. Nilisikia sauti za kupigana na muda mfupi kidogo Lulu alifungua mlango na kuja chumbani kwangu akasema, Kanumba amedondoka sijui amekuwaje


Alidai aliondoka hadi chumbani kwake, alimkuta Kanumba amedondoka kwa kuegemea ukuta huku akiwa hawezi kupumua, (amesafocate), alimchukua na kumlaza chini kisha akampigia simu Dr Paplas kulikuwa na alama mbili za nywele zilizokuwa zinaonyesha kuwa alipoburuzika,
Alidai, Mazingira ya chumba hicho cha kaka yake yalikuwa ya kawaida kama Siku zote.

alidai baada ya hapo aliwasha gari na kwenda kumchukua Dr ndipo Lulu akanipogia simu na kusema Kanumba haamki. Aisha Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alimuuliza Shahidi kama ushahidi aliotoa mahakamani unafanana na maelezo a logo to a by polisi alisema ndio,Kibatala alimuuliza shahidi huyo ni wapi aliwaeleza polisi kuwa alimuacha mshtakiwa Lulu peke yake Marehemu Kanumba wakati anaenda kumtafuta Dr, Paplas alisem hakuwaeleza.

Akaongeza kuwa yeye alikuwepo kwenye postmotam ya kawaida na wala hakuwepo wakati wakichukua sampuli za mwili kupeleka maabara.
Kesi itaendelea kesho.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE