
Mrembo Julitha Kabete (Katikati) mara baada ya kushinda taji la miss Ilala mwaka jana.
……….
Na Mwandishi wetu
Uongozi wa Kampuni ya Lino
International Agency Limited ambayo inaandaa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania imemteua Julitha Kokumanya Kabete kuwaikilisha Tanzania
katka mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika Sanya, nchini China
mwezi ujao.
Afisa Habari wa Lino
International Agency Limited, Hidan Ricco amesema kuwa tayari jina la
mrembo huyo limekwishwa wasilishwa kwa waandaaji wa mashindano hayo
yaliyopangwa kufanyika Novemba 18, kwenye ukumbi wa Crown of Beauty
Theatre.
Ricco amesema kuwa mrembo huyo
ambaye ni ambaye ni mshindi wa shindano la Miss Dar Centre, Miss Ilala
na mshindi wa tano wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka jana, kwa sasa
yupo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo.
Alisema kuwa uteuzi wa Mrembo
Julitha Kabete umezingatia uzoefu wa mashindano ya urembo alionao, uwezo
wake katika Tasnia ya urembo, uelewa wa vivutio vya utalii na raslimali
tulizonazo hapa nchini, pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyonayo
mrembo huyu tangu mwanzo anashiriki mashindano ya urembo ya Miss
Tanzania katika ngazi ya Kitongoji, Mkoa, Kanda hadi Fainali za Taifa
kwa mwaka 2016.
“Julitha pia alipata fursa ya
kushiriki mashindano ya urembo ya Afrika 2016 (Miss Afrika 2016)
yaliyofanyika nchini Nigeria na alituwakilisha vizuri tu, na hivyo
kupata uzoefu wa kutosha, jambo ambalo pia litaongeza uwezo wake wa
kutuwakilisha vema katika Mashindano ya urembo ya Dunia 2017,” alisema
Ricco.
Mashindano ya Miss Tanzania yanayoendelea katika sehemu mbalimbali ambapo fainali zake zitafanyika hapo baadaye.
Alisema kuwa mshindi wa mwaka
huu atawakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia hapo
mwakani 2018, hivyo kupata muda wa kutosha wa matayarisho.
“Hii sio mara ya kwanza kwa
mrembo wa Taifa wa mwaka huu kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya
Dunia mwaka unaofuata, mwaka 2012 Miss Tanzania Brigitte Alfred
aliwakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013,
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa aliwakilisha Tanzania katika
mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2014,” alisema Ricco.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE