October 25, 2017

Je uchaguzi wa marudio utafanyika Kenya?

Majaji wa mahakama ya juu nchini Kenya

Mahakama ya juu nchini Kenya leo Jumatano itasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa na wapiga kura watatu dakika za mwisho wakidai kuwa Kenya haiko tayari kufanya uchaguzi huo.

Mahakama imeombwa kuingilia kati na kuamua - iwapo uchaguzi wa marudio utafanyika..
Wanataka uchaguzi huo uahirishwe.

Rais Uhuru Kenyatta anasema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa siku ya Alhamisi.
Muungano wa upinzani chini ya kinara Raila Odinga umetaka wafuasi wake wasusie zoezi hilo, ukiutaja kuwa uchaguzi usioweza kuwa wa huru na wa haki.

Odinga amesema Serikali ya Kenya na tume ya Uchaguzi zimeshindwa kushughulikia mapungufu yaliyosababisha mahakama ya juu zaidi nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Agosti.
Hatua hiyo inajiri baada bya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.

 
Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.

Kumeshuhudiwa maandamano ya wafuasi wa upinzani wanaopinga uchaguzi huo wa marudio na wanashinikiza maguezi ndani ya tume ya uchaguzi IEBC na pia katika mfumo wenyewe wa uchaguzi.
 .................................................................................................................................................................
 KUWA  wa  kwanza  kupata  habari  za  mpya kupitia Chanel  zetu  za Daima TV na Matukiodaima katika Yotube ingia sasa  na  kisha bonyeza hapa  Subscribe

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE