October 9, 2017

JAFO AWAPA PONGEZI WANANCHI KISARAWE.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiipongeza kamati ya ujenzi kijiji cha Kwala wilayani Kisarawe kwa ujenzi wa madarasa mapya.
............................................................................
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewapongeza wananchi wa kisarawe kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ofisi za walimu, nyumba, pamoja na vyoo. 

Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua mradi ya ujenzi wa madarasa wilayani kisarawe katika vijiji vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala. 

Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake unafanyika kwa bora unaotakiwa. 

Kutokana na mwamko mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao katika kushirikiana na serikali na viongozi walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani wote wa kisarawe, Jafo amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE