October 9, 2017

IGP SIRRO ; SUALA LA TUNDU LISU LINAFANYIWA UPELELEZI NA HAWA WATU WASIOJULIKANA WATAJULIKANA TU

Mkuu wa  jeshi la  polisi nchini  (IGP)  Simon Sirro  akizungumza na wanahabari leo  mjini  Iringa  kushoto ni  kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa Julius Mjengi
Mkuu  wa  polisi nchini Simon Sirro  akipokelewa  leo
Na MatukiodaimaBlog
MKUU  wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema  kuwa   watu  wasiojulikana watajulikana baada ya  kukamatwa  na kuwa  suala la  mbunge wa jimbo la  Singinga  Mashariki Tundu Lisu linafanyiwa  uchunguzi na jeshi la  polisi kama  yalivyo matukio mengine.
 
Kuwa mtu anayepanga  kufanya uhalifu   huwa  hafiki  polisi  kujitambulisha  kuwa ana kwenda kufanya uhalifu ndio  maana akifanya  uhalifu anaitwa mtu  asiyejulikana  ila akikamatwa  hujulikana  .
 
“ Watu  wasio  julikana ni matumizi  tu  ya  lugha  ila  wakikamatwa  hujulikana na  hawaitwi  wasiojulikana  tena  ,tunaendelea  kuwasaka hao  wanaojiita  watu  wasiojulikana   hata  kule   Kibiti waliokuwa  wakifanya  mauwaji walikuwa ni   watu wasiojulikana baada ya  kuwakamata ni  watu  wanaojulikana “
 
 IGP  Sirro  aliyasema  hayo  leo mjini  Iringa wakati  akizungumza na wanahabari baada ya  kuwasili kwa   ziara  yake ya  kikazi  mkoani hapa, kuwa  suala  la Lisu kila  siku amekuwa  akiulizwa na  wanahabari kuhusu  upelelezi  wake  umefikia  wapi ila  kwao  jeshi  la  polisi  wanaliona  tukio  hilo ni  sawa na matukio  mengine .
 
“ mimi  sio  mwanasiasa  hili  ni  tukio kama yalivyo matukio mengine na Lisu  ni   mtanzania  kama  wengine  hivyo  jeshi la  polisi  linaendelea  kulifanyia  uchunguzi  suala  hilo kama yaliyo matukio mengine  ,kila  siku  maswali ni  juu ya Lisu ila  niwaambie  kuwa hili   ni  tukio la kama matukio mengine tunaendelea  na uchunguzi  “
 
Alisema  kuwa  suala  hilo la  Lisu  limekuwa  likizungumzwa kila  wakati  ifahamike  kuwa  suala  hilo  linafanyiwa kazi na kitengo  cha upelelezi na hategemei  kufundishwa kazi na mtu juu ya  nini afanye katika suala  hilo .
Hata  hivyo  alisema  kuwa kwa  upande  wake ana weledi ndani ya  jeshi la  polisi na haoni changamoto  yeyote  kufanya kazi na  wanasiasa  kwani  wanasiasa  mi  sehemu ya jamii na  wanafanya  siasa  kwa mujibu wa  sheria  ila wakikiuka sheria  wanawajibika kwa mujibu wa  sheria .
 
“  Kwa  hiyo  hakuna mwanasiasa  aliye juu ya  sheria  akiuka  sheria atawajibika kwamujibu wa  sheria  na  atashughulikiwa kama  mtu mwingine yeyote hivyo hakuna  mwanasiasa atakayenisumbua  mwanasiasa  atakayetoa  lugha ya  matusi atakamatwa  tu  kazi yangu ni rahisi  sana kwa  kuwa nasimamia  sheria .
 
 

Aidha  IGP  Sirro  aliwataka  askari wa  usalama  barabarani kutumia  busara  zaidi  katika kazi  hiyo badala ya  kuwapiga  faini madereva  pasipo kuwapa  onyo kuwa  kufanya  hivyo  si  sahihi .
 
Alisema pamoja ipo  dhana potofu  miongoni mwa jamii  kuwa askari  hao wa  usalama barabarani huwa wanapangiwa kiasi  cha pesa  kwa  ajili ya kukabidhi  kwa  siku jambo  ambalo si  kweli  kwani hakuna anayempangia pesa  za  kukusanya  askari zaidi ya  kumataka  kusimamia sheria  za  usalama barabarani .
 
“ Hakuna  askari wa  usalama  barabarani anayepangiwa makusanyo  ya  faini IGP ni   mmoja nchi  hii  mimi  ndio IGP nasema hakuna IGP anayepangia askari wa  usalama barabarani pesa labda wana IGP wao  nyumbani  kwao “
 
Kuwa kazi ya  askari  hao wa usalama barabarani ni  kusimamia  sheria  za  usalama barabarani na  sio  kila kosa  ni la kumpiga mtu  faini lazima busara  itumike  ikiwa ni pamoja na kumpa onyo mhusuka  pamoja na elimu kabla ya  kukimbilia  kumpiga  faini .
 
“  Jambo la  kwanza la  kuzuia  uhalifu ni  elimu kwanza siku ya  pili onyo na  siku ya  tatu ni faini  sio unaanza kwa faini  pasipo kumpa  elimu wala  onyo , ila  wakati  mwingine hawa  polisi  si malaika  yawezekana  wametoka nyumbani wakiwa ovyo  hivyo  wanahamishia hasira  zao kwenye  faini  ila naomba muwaelewe  hawa ni  watoto  wetu tuwasamehe bure ila ninachosisitiza elimu kwanza  ukiona dereva kaongeza  spidi kwanza  mpe  elimu kwanza ”
 
Kuhusu uboreshaji wa nyumba  za askari  polisi  nchini  alisema  kuwa kuna  programu maalum ya  kuboresha   makazi ya  askari  polisi kupitia  fedha wanazopata  .
 
“ Nimefurahi sana kuwafahamu  nimekuwa  nikisoma tu  nondo  zenu  ila   leo  nimewafahamu  ahsanteni  sana  ila naombeni  jaribuni  kuandika  kile ambacho  nimesema  kuna mmoja jana  Mbeya ameandika  IGP anasema wana Siasa  wasiongee hii si  kweli  mimi siwezi  kuwazuia  wanasiasa kuongea  wazungumze tu  ila  wasivunje sheria”

Kuhusu kauli  mbali  mbali ambazo  amekuwa  akiziandika kwenye  mitandao ya   kijamii Mange  Kimambe alisema kuwa kauli  zake  hizo zimekuwa  zikivunja  sheria  ndani ya  nchi  ila nini  ambacho  jeshi la  polisi  lina mpango  gani hawezi  kusema kwa  sasa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE