October 9, 2017

HOSPITALI YA KIMATAIFA YA MACHO YATOA PUNGUZO LA BEI KWA HUDUMA YA MATIBABU YA MACHO.

KUELEKEA siku ya uoni Duniani Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa punguzo la bei za matibabu kwa asilimia 25 kwa watu ambao wataenda kutibiwa katika hospitali iliyop jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima amesema kuwa hospitali ya Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa huduma za upasuaji wa macho kwa gharama nafuu sana.


Amesema kuwa kwawatu wenye bima za afya wanaweza kwenda kutibiwa katika hospitali hiyo kwa wale wenye bima za afya waliojiunga na hospitali hiyo hasa wenye bima za Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) pamoja na mifuko mingine.
 Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa hospitali hiyo ya Kimataifa ya macho inapunguzo la bei kwa watakaoenda kutibiwa watapata punguzo la bei kwa pia kwa wale wenye bima ya afya watatibiwa kuitia bima zao. Kulia ni Meneja Masoko wa Hospitali ya Kimataifa ya Macho(The International Eye Hospital),Ilakoze Bidyanguze. 

 Daktari Bingwa wa upasuaji wa Macho wa hospitali ya kimataifa ya macho(The International Eye Hospital), Adyn Buren, Muuguzi wa (The International Eye Hospital), Denis Malanga, na Muuguzi wa hospitali ya Kimataifa ya macho (The International Eye Hospital), Ana Athanas wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa macho aliyeenda kutibiwa katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya miwani ambayo hutolewa na Hospitali ya Kimataifa ya Macho (The Intarnationa Eye Hospital)iliyopo jijini Dar es Salaaam wa wale ambao wataenda kutibiwa katika hospitali hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE