October 4, 2017

BUNDUKI ZILIZOPO DUNIANI ZINAWEZA KUWAUWA BINADAMU WOTE KWA KUWAPIGA RISASI ZAIDI YA MOJA


Tukio la mauaji ya watu wapatao nchini 58 nchini Marekani na wengine mamia kujeruhiwa limeibua mjadala wa umiliki wa silaha za moto duniani kote.
Muuaji Stephen Paddock alikutwa na bunduki za kivita 23 katika chumba cha hoteli ya Mandalay katika jiji la Las Vegas alipotelekeza uhalifu huo na kisha kujiua kabla ya kukamatwa.
Silaha nyingine za kivita 19 zilikutwa katika moja ya nyumba zake na kuzua mjadala juu ya umiliki wa silaha kwa raia.
Utafiti uliofanywa na Shirika la GunPolicy la nchini Australia unaonyesha kuwa duniani kote kuna takribani silaha za moto 885 zinazomilikiwa kihalali pamoja na risasi za kutosha kumpiga mtu zaidi ya mara moja.
Marekani pekee inadiriwa kuwa na zaidi ya silaha za moto milioni 220 zilizopo mikononi mwa raia wake kihalali na kuifanya nchi namba moja kwa umiliki binafsi wa bunduki.
Kuhusu Tanzania
Mtandao huo unaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya silaha 100,000 zikiwamo zile zinazotengenezwa kienyeji.
Ripoti hiyo inaitaja Tanzania kushika nafasi ya 137 kati ya nchi 178 zenye umiliki wa silaha za moto kwamba silaha zilizosajiliwa mpaka kufikia mwaka 2012 zilikuwa chini ya 69,000.
Hata hivyo inasema hakuna tishio la matumizi au utengenezaji wa silaha wa kushtua ukilinganisha na mataifa mengine.
Pia, unaitaja Tanzania kujitahidi kwa kujiunga na mikataba mbalimbali ya kudhibiti matumizi ya silaha na utengenezaji kiholela.
Wakati akiwasilisha bajeti yake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema katika kupambana na wimbi la umiliki haramu wa silaha nchini Jeshi la Polisi lilianzisha uhakiki wa silaha mwezi Machi, 2016 ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2017 asilimia 63.20 ya silaha zilizosajiliwa zilikuwa zimehakikiwa.
Katika uhakiki huo jumla ya silaha 486 zilisalimishwa kutokana na kutomilikiwa kihalali ambazo ni bastola - 16, rifle - 18, shotgun - 161, SMG - 24, G3 - 1 na magobore 266 katika mikoa mbalimbali nchini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE