October 21, 2017

ASKOFU MSTAAFU KKKT IRINGA AWASHUKIA WANAOTAKA KATIBA MPYA

HUKU ikiwa ni  siku  chache toka  mmoja  wa Chama  cha Mapinduzi (CCM) kutoa kauli ya  kutaka Rais Dkt John Magufuli kuongezewa muda wa kubaki madarakani kutokana na kazi nzuri anayoifanya ,askofu mstaafu  wa kanisa la  kiinjili la  kilutheri Tanzania (KKKT)  Dayosisi ya Iringa Dkt Owdenberg Mdegela  ameibuka  na  kutaka wote wenye mawazo kama  hayo kufuta na kutaka katiba iheshimiwe.

“ Hakuna  asiyetambua  vita  kubwa  ambayo Rais Dkt Magufuli ambayo anaifanya  vita  ya  kupambana na wezi  wa raslimali  za  nchi  hii na mafisadi hii  ndio vita tunayoitaka na  tunamuunga mkono  ila sasa  hawa  wanaoibuka kusema aongezewe  muda wa kukaa madarakani ili  iweje  katiba  yetu  ipo  wazi  ni vipindi viwili  vya miaka  mitano  mitano si  vinginevyo”

Dkt  Mdegella  aliyasema  hayo  jana  wakati  wa mahojiano maalum na mtanzania mara  baada ya  kumalizika kwa ibada  maalum ya  ufunguzi  wa mkutano wa  Lutheran Mission  Cooparation (LMC) uliofanyika kidunia mkoani Iringa.

Akizungumzia  kuhusiana na mchakato  wa katiba  mpya  alisema kuwa kwa  moyo  wake  wa dhati  kuwa katiba  mpya  si  kipaumbele cha  sasa kipaumbele chake ni  kuendelea  kuwakamata  wezi  wa madini na wengine  ambao  walikuwa  wakifanyia  vikao  vyao  Dubai .

“ Tatizo la watu  wengi sasa  hivi  hawaangalii  mahali   tulipo kuwa jinsi  gani tulikuwa pabaya  hii katika  mpya  wamekula  pesa  nyingi ila bado  wanataka  kula  tena  wakati wizi umejaa mimi  sikubali  hata  wale  watakaosema  nimetofautiana na fulani sawa  tu  mimi  huo  ndio msimamo  wangu “

Alisema  kuwa  kilio cha watanzania  kwa  sasa  kuona  wanapata  ajira  na  kuwa na maisha  bora na  tayari  misingi ya  hayo  yote  serikali ya  awamu ya  tano  imeanza  kuyaweka  vema kwa  kuona wenye  vyeti  feki  waliokuwa wakiwakosesha  wenye elimu  kupata kazi  wanaondolewa  huku jitihada za  kuboresha  maisha ya  watanzania zikiwekewa  mfumo mzuri ukiwemo  wa kuwafanya  watanzania  wote kunufaika na  uchumi  wa  Taifa   hili .

  Watu  wanaipiga  kelele  kutaka katiba  mpya kwa maoni  yangu  kwa  sasa  tumuache Rais Magufuli kutengeneza mfumo  mzuri  wa maisha  bora  kwa  kila mtanzania  kwa  kuwabana  wezi  na mafisadi katika nchi  hii akituondolea  hawa  tutafaidi  mema ya  nchi  wanaotaka  Rais  Magufuli  kuongezewa  muda hao   hawajitambui lazima  tufuate katiba  yetu  inasemaji  ni miaka 10  hivyo kama hivyo  ndivyo  ikiisha  miaka  mitano  basi wajitokeze kumchagua  tena ili  ifike  miaka  10  baada ya hapo katiba  hairuhusu”

Alisema  kuwa Mwalimu Julius  Nyerere  alikaa miaka 25 ila  bado  matatizo ya  kiuchumi  yaliendelea  kuwepo  pamoja na kazi  kubwa  aliyoifanya ambayo  inakumbukwa  hadi  leo na  baada ya  hapo  aliingia Alli Hassan  Mwinyi  akaweka mabadiliko nayo yakawa na matatizo  yake kabla ya  kuja  Benjamin Mkapa pia  alimaliza  miaka  yake 10 hivyo  nchi  yetu katiba  ipo  wazi madarakani  kwa  Rais ni  miaka  10  si  vinginevyo.
 
Dkt  Mdegella  alisema jambo la  watanzania  kuendelea  kufikiri  kwa  sasa ni namna gani watakuja  kumpata Rais mzuri kama Dkt Magufuli  pindi  muda  wake  ukimalizika kwa  mujibu wa katiba ili  kazi  hii nzuri ya  kupambana na majambazi na mafisadi  wa Taifa  hili na  wanaopandikiza ugaidi iweze  kuendelezwa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE