October 10, 2017

ALIKIBA-NINAMUHESHIMU MANGE KIMAMBI

Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Seduce me' amefunguka na kusema kuwa Tanzania kila mtu ana haki na uhuru wake hivyo hata yeye anajisikia vizuri kuona watu maarufu wanapenda kazi zake na kudai ana haki ya kupendwa na Mange Kimambi
Alikiba amedai kuwa Mange Kimambi ni moja kati ya mashabiki zake na kusema anashukuru sana kuona anapenda kazi zake na kumpa nguvu katika kazi zake hizo kwa kutoa 'support'.
"Ni kama shabiki wangu na 'appreciate' anapenda muziki wangu kwa sababu mimi namuheshimu kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anani 'support' kwenye kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru hivyo kila mtu ana haki na vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yoyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia" alisema Alikiba 
Mbali na hilo Alikiba alisema anajisikia vizuri kuona muziki wake unazidi kufika mbali zaidi duniani na kuendelea kufanya vizuri nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla.
"Najisikia furaha zaidi pale napoona watu wanaojulikana na maarufu nao wanafurahi na muziki wangu na si kusikia muziki tu bali ni mashabiki wangu pia, hivyo kwangu mimi ni raha sana, nawapenda sana mashabiki zangu wote duniani kwani nyinyi mnanipa furaha na amani" alisema Alikiba 
EATV

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE