October 16, 2017

ALICHOKIZUNGUMZA MKE WA DEO FILIKUNJOMBE KWENYE MIAKA MIWILI YA KIFO CHAKE

Ikiwa ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe afariki dunia, mke wa wake Sarah Habiba amesema Tanzania ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, huku wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu.
"Mume wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi wangu, ntakukumbuka daima mpenzi", ameandika Sarah Habiba.
Deo Filikunjombe alifariki Octoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta iliyoanguka kwenye msitu wa hifadhi ya Selous akitokea Dar es salaam kwenda Ludewa, nakiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera ambao pia walifariki dunia.
Deo Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa na wabunge wengine, akiwemo rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Alichokiandika mke wa Filikunjombe instagram

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE