September 6, 2017

WAZIRI JAFO AWATAKA WATAALAM WA LISHE KUFIKISHA ELIMU YA LISHE KWA JAMII.Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewataka wataalam wa lishe nchini kufikisha elimu ya lishe kwa jamii kwa lugha nyepesi ya kiswahili katika jamii.

Jafo aliyasema hayo wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa siku mbili wa wataalam wa mambo ya lishe uliokuwa ukilenga suala la urutubishaji wa vyakula hapa nchini.
 Mkutano huo wa kitaifa ulifanyikia Dar as salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Nyerere ambapo wataalam wa lishe, watafiti, wadau wa maendeleo, wamiliki wa Viwanda vya kurutubisha vyakula, pamoja na wananchi walishiriki.

Akizungumza katika mkutano huo, Jafo alitoa angalizo kwa wataalam na watendaji kutumia lugha isiyo rafiki kwa wananchi (lugha ya kiingereza) wakati wa kujadili na kufikisha elimu ya lishe.

Jafo amesisitiza matumizi ya lugha ya kiswahili ili wananchi walengwa wa elimu hiyo waweze kufahamu nini kinajadiliwa na namna ya utekelezaji wake ili kufanikisha mapambano dhidi ya tatizo la utapiamlo hapa nchini.

Aidha, Jafo amezitaka taasisi zinazosimamia ubora wa vyakula ( TBS na TFDA) kuongeza ufanisi wa usimamizi wa bidhaa ili viwanda vinavyorutubisha vyakula vitekeleze wajibu wao na wasisite kuwachukulia hatua wale wote wataokiuka utaratibu.

Amesisitiza urutubishaji wa chumvi kwa kuweka madini joto sambamba na urutubishaji wa unga wa mahindi, ngano na mafuta ya kula.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE