September 6, 2017

WATENDAJI MANISPAA YA KIGAMBONI WAPONGEZWA

Image result for waziri Jafo
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza watendaji wa Manispaa ya Kigamboni kwa moyo wao wa kujituma katika kuitumikia manispaa hiyo mpya.

Jafo ametoa pongezi hizo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kuzungumza na watumishi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa mabweni, madarasa, maabara na vyoo katika shule ya sekondari ya Somangira ambapo serikali ilipeleka sh. milioni 259 ili kujengwa miundombinu hiyo na kufanya shule iwe na uwezo wa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano waliochaguliwa kwa awamu ya pili.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea hospitali ya Vijibweni na kuwamwagia sifa watendaji wote wa hospitali hiyo kwa usimamizi mzuri kwa kuwa na mazingira ya usafi wa kuvutia.

Hata hivyo Jafo alielekeza kutenga eneo Maalum kwa ajili ya duka Maalum la wagonjwa wa bima ya afya ili wagonjwa wote wa bima wasikose dawa wanapofika hospitalini kupata matibabu.

Naibu Waziri huyo pia amempongeza Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi wote wa wilayani kwa kazi nzuri ya usimamizi wa wilaya hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE