September 6, 2017

WANAUME CHANZO CHA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI ..

Mwakilishi  wa  EKAMA   Development  Foundation  Tanzania   , Lucia  Akaro akitoa  mada  leo katika  ukumbi wa  TGNP  Mtandao  mabibo  jijini Dar es Salaam
Washiriki  wa  warsha  wakifuatilia  warsha  hiyo
Mada  ya  ardhi  ikitolewa
BAADHI  ya  wanaume  nchini  wametajwa kuwa ni  chanzo  cha  migogoro ya ardhi na ukatili  wa  kijinsia  katika familia  zao  kutokana na tabia za  kuendekeza starehe  wakati  wa mavuno kwa  kukimbia familia  zao na kutumia  pesa  za mavuno  na  vimada .
   

Akiwasilisha  mada   ya  ardhi ,kilimo ,uzinduaji  ,uchimbaji madini na mabadiliko  ya  tabia  nchini  kwa  wanawake  na makundi yaliyoko pembezoni  leo wakati  wa  warsha  zinazoendelea  katika tamasha la 14  la mtandao  wa   jinsia  Tanzania (TGNP – Mtandao ) mwakilishi  wa  EKAMA  Development  Foundation  Tanzania   , Lucia  Akaro  alisema  kuna  haja ya  mifumo kandamizi  kwa  wanawake  kukemewa .

Kwani  alisema  kuwa changamoto  za migogoro ya  ardhi na manyanyaso  kwa  wanawake  hujitokeza  wakati  huo  wa mavuno  kwa baadhi ya  wanaume  kutumia  fedha  za  mavuno  kwa  kuongeza  mke  wa  pili ama  kuendekeza  starehe  huku  familia ikiteseka .

“Kundi la wanawake ndilo kundi linaloathika zaidi na mabadiliko ya Tabianchi  Katika  kupambana na  ukatili  wa  kijinsia  kuna haja  ya  kuanzisha  majukwaa mbali  mbali ya  utoaji  wa  elimu  kwa  jamii  kuondokana na unyanyasaji  wa  familia kupitia  ardhi ama mavuno “

Alizitaja  athari zitokanazo na ukatili wa jinsia ni pamoja na Kupungua kwa nguvu kazi pamoja na kipato cha wanawake kinachopelekea kuwepo kwa umaskini ,Kupungua kwa uhifadhi wa chakula (usalama wa chakula,Kupotea kwa haki ya mwanamke kumiliki ardhi na upatikanaji wa ardhi  na Kukosekana kwa muda wa kutosha kufanya kazi shambani kutokana na vitendo vya kikatili .

Hivyo alisema Katika kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya kilimo  kuna haja  ya  kuwajumuisha  wanawake  katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili kungeza bei ya mazao na kuteneneza nafasi nyingi za ajira .

Aidha  alisema kuna haja ya kuongeza jitiada katika kuzuia upotevu wa mazao kipindi cha uvunaji na baada ya uvunaji kwa kuhifadhi  mazao vizuri katika maghala au katika mapipa maalum  na Serikali iongeze bajeti katika sekta ya kilimo na bajeti iwe na mlengo wa kijinsia, pia ugawaji wa fedha ufanyike kama ilivyokusudiwa


“Ni muhimu sana kujumuisha masuala ya mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi ngazi ya taifa elimu itolewe kwa jamii kuhusu athari za ukatili wa jinsia Wanaume wahusishwe katika mapambano ya kupinga ukatili wa jinsia kwakua tafiti zinaonyesha hao ndio chachu ya ukatili wa jinsia Wanawake wawezeshwe zaidi na  kupewa fursa za kushiriki maamuzi na mipango mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii “

Washiriki  wa  warsha  hiyo  Nembris Mollel  na Zainabu kamili  walitaka  asasi  zinazoshughulika na harakati za  kumkomboa mwanamke  kuiga mfano  wa TGNP Mtandao  kwa  kuwatembelea  wananchi wa  pembezoni  mwa  nchini  badala ya  kujikita  mijini pekee.

Kwani  walisema wanawake na watoto  wengi  wanaoteseka  juu ya  ardhi  ni wale  wa  vijijini ambao  hawajafikishiwa  elimu  ya kutosha ya  kupambana na  wanaume  wenye  tabia  za  manyanyaso.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE