September 29, 2017

WALCOTT APIGA MBILI ARSENAL IKIITWANGA 4-2 BATE BORISOV EUROPA LEAGUE

Wakicheza bila ya mastaa wake timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya wenyeji Bate Borisov mchezo wa Europa League na kuwafanya vijana wa Mzee Wenger kuongoza msimamo wa kundi wakiwa na alama sita kwa mechi mbili walizocheza.
Mshambuliaji Theo Walcott kama angekuwa makini leo angeondoka na hat trick kutoka na kupata nafasi nyingi za kufunga ambapo ilimpelekea kufunga magoli mawili peke yake dakika ya 9 na 22 huku beki kinda Roy Holding akifunga la tatu dakika ya 25 hadi mapumziko Arsenal walikuwa mbele.
Kipindi cha pili wenyeji waliingia kwa kulishambulia lango la Arsenal kama nyuki na kuwafanya kupata goli la pili dakika ya 67 likifungwa na Gordeichuk na Oliver Giroud alifunga goli la nne na la ushindi.
Kwa Matokeo hayo Arsenal wamefikisha jumla ya pointi 6 na kuongoza msimamo wa Ligi hiyo huku Bate na Koln ya Ujerumani zikishika nafasi za mwisho.
VIKOSI:
Bate Borisov (4-2-3-1): Scherbitshi 4; Rios 6, Gaiduchik 5, Milunovic 4.5, Polyakov 4 (M Volodko 23, 6); A Volodko 5 (Baga 85), Dragun 4.5; Gordeichuk 6.5, Ivanic 7, Stasevich 5; Rodionov 5 (Signevich 54, 6)
Subs not used: Veremko, Yablonski, Berezkin, Tuominen
Goals: Ivanic 28, Gordeichuk 67
Yellow cards : Dragun 49, Milunovic 64, Ivanic 87
Arsenal (3-4-2-1): Ospina 7; Mustafi 6.5, Mertesacker 6.5, Holding 6.5; Nelson 7 (McGuane 79), Willock 7 (Nketiah 89), Elneny 6, Maitland-Niles 6; Walcott 7.5, Wilshere 8; Giroud 6.5.
Subs not used: Macey, Akpom, Dasilva, Dragomir, Gilmour
Goals: Walcott 9, 22, Holding 25, Giroud 49 
Referee: Daniel Stefanski (Poland)
MOM: Jack Wilshere 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE