September 18, 2017

UPELELEZI UMEKAMILIKA KESI YA AVEVA,KABURU

WhatsApp Image 2017-08-30 at 11.59.51

KESI inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu upelelezi wake umekamilika na jalada lao limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa ili kuona kama ushahidi unajitosheleza.
Kesi hiyo iliyotajwa leo Mahakamani Kisutu, mbele ya Hakimu Victoria Nongwa, imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu itakaposikilizwa.
Aveva na Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
Upelelezi uliokuwa unafanyiwa kazi ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa kwa mtaalam kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE