September 19, 2017

UCHAGUZI WA KENYA HUENDA UKASOGEZWA MBELE TENA


Uchaguzi mpya wa urais nchini Kenya huenda ukaahirishwa kutoka tarehe 17 mwezi ujao.
Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imekuwa ikikutana kuangalia uwezekano wa kuahirisha Uchaguzi huu baada ya kampuni ya Ufaransa ya Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.
Mbali na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga, umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.
Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE