September 5, 2017

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KENYA YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI WA MARUDIO

Wafula Chebukati
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

"Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw Chebukati imesema.

Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi.
Majaji wa tume hiyo hawakuandaa uchanguzi huo kwa viwango vilivyowekwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi, na kwamba kulitokea kasoro nyingi sana katika mchakato wa kupeperusha matokeo.
Image caption Rais Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ndio pekee watawania
Bw Chebukati amesema tume hiyo inafanyia utathmini mifumo na taratibu zake kwa ajili ya uchaguzi huo mpya.

Mwenyekiti huyo hata hivyo ametoa wito kwa Mahakama ya Juu kutoa hukumu ya kina kuhuhusu kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga kupinga ushindi wa kenyatta ili kuiwezesha "tume kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa katika usimamizi wa uchaguzi mpya".

Majaji wa mahakama ya juu waliahidi kutoa hukumu kamili kabla ya tarehe 22 mwezi huu.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na IEBC kuhusu uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Upinzani ulipinga matokeo hayo ukisema mitambo ya tume hiyo ya uchaguzi iliingiliwa kumfaa Bw Kenyatta
IEBC ilikuwa na muda wa hadi tarehe 31 Oktoba kikatiba kuandaa uchaguzi mpya.

Lakini waziri wa elimu alikuwa ameomba tume hiyo kuandaa uchaguzi huo mapema ili kutovuruga mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne ambayo imepangiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa Oktoba.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE