September 20, 2017

TIMU YA MAJI MAJI NI MAJI YA SHINGO YATEMBEZA BAKURI


Uongozi wa Klabu ya Majimaji yenye makao makuu Songea Ruvuma Tanzania siku ya tarehe 19 /09/2017 ilitoa namba maalumu kwa ajili ya wadau mbalimbali wakereketwa,wanachama na wapenzi wa Klabu hiyo popote walipo Tanzania kuweza kuichangia kwa kiwango chochote ambacho watajaliwa nacho ili kuiwezesha kujiendesha katika ligi kuu Tanzania bara.

Pamoja na mengine yote Klabu imeona ni bora ibuni njia mbalimbali za kuweza kujipatia kipato ili iweze kujiendesha vyema, na hii ni kutokana na hali ya ukata iliyokuwa nayo.

Klabu ina vyanzo kadhaa vya Mapato ikiwemo jezi za Mashabaiki ambazo zipo mtaani hivi sasa na bado uongozi unaendelea kutafuta Vyanzo mbalimbali vya mapato na wadhamini mbalimbali pia ili Klabu iishi vizuri.

Tunashukuru sana Uongozi wa Sokabet kwa kukubali kutudhamini kwa mkataba wa mwaka mmoja,Sasa hapa kuna baadhi ya wadau mbalimbali kama panawachanganya kidogo,Sokabet wao wamechukua Upande wa Mishahara kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kwa mwaka huo mmoja,Sasa Kama bodi bado ina kazi ya kufanya maanake kuna uendeshaji mwingine katika Klabu kama vile kambi,Chakula,Safari n.k
Kwakuona hilo kama uongozi ukabuni vyanzo vingine vya mapato huku wakiendelea kutafuta udhamini mwingine katika sehemu mbalimbali.

Mwisho nawashukuru waandishi wenzangu wa habari kwa ushirikiano mnaonipa.Mungu wabariki sana katika kazi zenu.

wadau na wapendwa wote wanaweza kuchangia kupitia 0744000262 NA 0785212253 ,JINA LITATOKEA MAJIMAJI FOOTBALL CLUB.
Imetolewa na idara ya habari na Mawasiliano ya Majimaji.
Onesmo Emeran Ndunguru.0712 904205 Au 0623862256.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE