September 27, 2017

TANAPA: INAKUPELEKA KUTALII HIFADHI YA RUAHA KWA 30,000/- TU KWENDA NA KURUDI

Na Friday Simbaya, Iringa
Wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini wameaswa kutumia fursa ya siku mbili maonesho ya utalii karibu kusini kuitembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha iliyopo wilayani Iringa, mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habri ya meneja masoko wa shirika la hifadhi za Tanzania (TANAPA) aliwaomba wananchi kutumia siku mbili za maonesho ya utalii yanayofanyika kwa wiki moja mjini iringa kwenda hifadhi ya ruaha kwa gharama nafuu.

Alisema kuwa TANAPA kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini intenga siku mbili maalumu kwa ajili wananchi kwa ajili ya wananchi kutembelea hifadhi hiyo kwa gharama nafuu katika ya septemba 28 -30 mwaka huu.

“Kwa kupitia ofa hiyo kutakuwa na mchango mdogo wa fedha; mtu mzima atalazimika kuchangia Sh 30,000 na mtoto Sh 10,000 tu kumuwezesha kwenda kwa siku moja kutalii katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini,” alisema.

Alisema mchango huo unahusisha gharama ya usafiri, kiingilio cha hifadhini, utalii na muongoza wageni atakayewapitisha katika vivutio mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo.

“Tuna nafasi 50 tu tumetoa kwa kupitia ofa hii. Safari ya kwanza itahusisha watu 25 na safari ya pili watu 25 pia, kwahiyo wanaotaka wafike na kujiandikisha katika banda letu lililopo katika viwanja vya Kichangani yanapofanyika maonesho haya,” alisema.

Akizungumzia baadhi ya vivutio vilivyoko katika hifadhi hiyo, Mhifadhi wa Idara ya Utalii Ruaha, Hellen Mchaki alisema Hifadhi ya Ruaha pamoja na wingi wa vivutio inabeba pia historia muhimu ya Chifu Mkwawa, kiongozi wa kabila la Wahehe mkoani Iringa aliyeongoza mapambano dhidi ya wajerumani katika karne ya 19.

Alitaja baadhi ya wanyama waliopo katika hifadhi hiyo kuwa ni kudu wakubwa na wadogo, viboko, mamba, pofu, swala pala, makundi makubwa ya samba, tembo na nyati, chui, mbweha, fisi, twiga, pundamilia na mbwa mwitu.
\
Akizungumzia idadi ya watalii katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Mchaki alisema mwaka 2012/2013 walipokea watalii wa nje 14,299 na wa ndani 9,094, mwaka 2013/2014 wa nje 13,489 na wa ndani 9,673 na mwaka 2014/2015 wa nje 13,272 na wa ndani 8,291.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE