September 1, 2017

TAASISI YA KIISLAM YA DHI NUREYN YACHINJA NG'OMBE NA MBUZI KUWAPA MASKINI KUSHEREKEA EID


waumini  wa dini  ya  kiislam mkoa  wa  Iringa  wakishiriki  kuchinja ng'ombe leo
Sehemu ya  nyama  iliyochinjwa  ikisubiri  kutolewa  msaada  wa wananchi  wenye uhitaji
Zoezi la  uchinjaji wa  ng'ombe ukiendelea  mjini  Iringa leo

Taasisi ya kiislam mkoa  wa Iringa ya  Dhi Nureyn imetumia  kiasi cha  shilingi  milioni 20  kununua ng'ombe 13 na  mbuzi 90 kwa ajili ya kuwapa msaada  watu  wasio na uwezo kwa  ajili ya  kusherekea  sikukuu  hiyo ya Eid .

Katibu  wa Dhi Nureyn Iringa Shams  Elmi alisema kuwa  fedha  hizo zimetokana na  sadaka  zilizotolewa na  waumini mbali mbali wa  dini  hiyo  kwa ajili ya  kununua  mbuzi na  ng'ombe ili  kuwawezesha  wasio na uwezo wa  kuchinja kupata kushiriki  sikukuu  hiyo kama  wenye uwezo.


Alisema  ng'ombe 13 na  mbuzi 45  zimechinjwa  Iringa wakati mbuzi 45  zimesafirishwa kwa  ajili ya uchinjwaji  kama  huo mkoani Dar es Salaam .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE