September 22, 2017

SIKU YA AMANI DUNIANI , RC DODOMA ATAKA JAMII KUENZI AMANI

Mkuu wa wilaya ya Kondoa akisoma hotuba ya RC Dodoma 
DC Kondoa Sezaria V Makota akito cheti cha pongezi kwa RPC DodomaSERIKALI  mkoani Dodoma imeitaka  jamii kuendelea  kuipigania amani ili  kulifanya Taifa  kuendelea  kuwa  kisima  cha amani .

Wito  huo umetolewa leo  wilayani Kondoa mkoani  Dodoma na mkuu  wa  mkoa  huo  Jordan Rugimbana  wakati wa maadhimisho ya siku ya amani  Duniani kuwa  kuna maeneo duniani yako kwenye migogoro na machafuko yanayogharimu maisha ya watu, kusababisha uharibifu wa mali na kurudisha nyuma maendeleo.

“Ni jukumu letu sote kuwasaidia walioko kwenye migogoro kurejesha amani ili tuweze kutekeleza kwa pamoja malengo ya maendeleo endelevu naungana na Bw. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu  Mstaafu wa Umoja wa Mataifa aliposema kwenye hotuba yake ya tarehe 16 Septemba 2016 kuwaomba wapiganaji wote duniani kuweka silaha zao chini, kurejesha amani na kuunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu yanayoweka mpango kamilifu utakaotusaidia kuondokana na mizizi ya migogoro”

Alisema  kuwa amemefurahishwa na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu kitaifa isemayo

Hamasisha  Michezo tujenge Umoja,  Pamoja Kudumisha Amani, Heshima, Usalama na Utu kwa wote: #Amani ni fursa# kwa Maendeleo ya Viwanda Tanzania inaakisi moja kwa moja matakwa ya kila mmoja wetu na Taifa kwa ujumla ya kujenga na kuendeleza Umoja, Haki, Heshima, Utu kwa watu wote  ili kulinda na kudumisha  Amani ambayo kwetu ni fursa kwa  ustawi wa Maendeleo ya kila mmoja wetu na taifa”

Hivyo  alisema  kuwa anayo furaha kubwa kuungana na  wadau wa amani nchini katika kuadhimisha siku ya Amani Duniani.

“ Napenda kutumia nafasi hii ya kipekee kutoa shukrani zangu za dhati kwa Ofisi ya Kituo Cha Amani Haki na Msaada wa Kisheria Tanzania  pamoja na ASASi za kiraia zote zilizoshiriki kuandaa na kunialika kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho haya muhimu kwa ustawi wa Taifa na Dunia kwa ujumla, ni ukweli usiopingika kuwa Michezo ni nguzo pekee ya kuwaleta  pamoja watu wote bila kujali Dini, Rangi, Rika,Jinsia, Itikadi wala kabila ikiwa ni ngao ya kutuunganisha watanzania  wote  kukutana na kujenga mahusiano mema na kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya ustawi wa jamii na kudumisha Amani, Heshima, Utu na  Umoja ni chanzo kikuu cha kumaliza migogoro ya kijamii kote ulimwenguni, Tukilinda Amani na utulivu vilivyopo itakuwa njia na misingi ya kufanikiwa malengo ya serikali ya viwanda nchini”

Mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  kuwa iwapo watanzania wasipochukua hatua sahihi Kulinda na kudumisha Umoja wetu na Heshima na utu  itakuwa vigumu  kukaa pamoja kama ndugu, na Migogoro itatamalaki na kuvuruga amani yetu tulioilinda kwa nguvu nyingi mpaka kufika leo.


“Migogoro isiyo isha katika jamii sio jambo la mzaha hata kidogo. Tuitokomeze  kudumisha amani yetu kama mnavyofahamu mwaka 2015 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Ajenda Mpya ya Maendeleo Endelevu iliyoanza kutekelezwa mapema mwaka huu ajenda hiyo yenye malengo 17 ni Dira ya maendeleo ya Ulimwengu kwa kipindi cha miaka 15 ijayo Pamoja na mambo mengine, malengo haya yanalenga kutokomeza umaskini uliokithiri, kupambana na matabaka na ukosefu wa haki.”

Kwa kutambua umuhimu wa Amani katika kuleta maendeleo, lengo namba 16 katika malengo hayo limejikita katika kujenga  jamii yenye amani na umoja kwa maendeleo endelevu; kutoa upatikanaji wa haki kwa wote na kujenga ufanisi, uwajibikaji na umoja wa taasisi katika ngazi zote. Kama nchi, tumehakikisha kuwa kuna utaratibu wa kukuza viwango vya maadili na kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanatambua wajibu wao wa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa umma.

Alisema wakati  Tanzania  inaungana  na nchi nyingine kuadhimisha siku ya amani Duniani  wanatambua  na kushukuru Umoja wa Mataifa kwa kulitambua hili, nchi yetu inaahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuhakikisha lengo hili linafanikiwa kujenga na kuimalisha Heshima, Usalama na Utu kwa wote kupitia uhamasishaji wa michezo  ambayo ni nguzo ya kutuweka pamoja na kutujengea upendo wenye  maono ya kudumisha amani nchini na kwingineko. Ni faraja kuwa tunaendelea kushirikiana vyema na jumuiya ya kimataifa katika kutimiza wajibu wetu tulioukubali kwa pamoja ili kuleta maendeleo endelevu.

“kwa kutambua umuhimu wa Michezo kama nguzo ya kujenga Afya, Amani na Maendeleo kupitia umoja unaohamasishwa kupitia michezo, Serikali ya Awamu wa Tano iliazimia na imetekeleza azma ya kuhamasisha Michezo nchini kote kupitia Mhamasishaji Mkuu Mheshimiwa  Makamu wa Rais Samia Hassani Suluhi aliye zindua na kuamasisha  wanachi wote kuungana na Serikali kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimalisha Afya, Kudumisha Amani na maendeleo

Kuwa  vijana ndio nuru kubwa ya Taifa pia ni viongozi wa kesho Wanapaswa kuwa mahiri, makini na wenye kuipenda na kulinda amani. Kutoweka mkazo katika umuhimu wao inaweza kuleta matatizo.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa vijana wengi  ni wepesi wa  kudanganyika na hivyo kuingia kwenye shughuli ambazo hazina manufaa na zenye madhara kwa jamii. Aidha, wazazi hatuwezi kubaki nyuma. Inapaswa tushirikiane ili kujenga misingi ya uzalendo na amani katika ngazi ya familia. Suala hili likizingatiwa taifa litanufaika kwa kuwa na mahali salama na penye kustawisha maendeleo ya kila mmoja wetu.

Kwa  upande  wake  mwakilishi wa NGOS   mkurugenzi wa Kituo cha Amani Haki na Msaada wa Kisheria Tanzania (PLAJC) Bw Jaruo B Karebe akitoa neno la  shukurani kwa  mkuu  huyo  wa  mkoa alisema  kuwa maadhimisho  haya  ya siku ya Amani  Duniani yameandaliwa kipekee na baraza la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuhakikisha dunia inakuwa mahali salama pa kuishi, kutokomeza umaskini, kutokomeza vitendo vyote vya uvunjifu wa haki za binadamu na kukuza mahusiano yanayoleta na kujenga amani.

Kwa mkoa wa Dodoma  maadhmisho haya yanafanyika wilaya ya  Kondoa na waandaaji wa siku hii ni Kituo Cha Amani hai na Msaada wa Kisheria Tanzania (PLAJC)  kwa ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Dodoma  pamoja na asasi nyingine zisizo za kiserikali.

“nimefurahishwa na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu kitaifa isemayoHamasisha  Michezo tujenge Umoja,  Pamoja Kudumisha Amani, Heshima, Usalama na Utu kwa wote: #Amani ni fursa# kwa Maendeleo ya Viwanda Tanzania ”inaakisi moja kwa moja matakwa ya kila mmoja wetu na Taifa kwa ujumla ya kujenga na kuendeleza Umoja, Haki, Heshima, Utu kwa watu wote  ili kulinda na kudumisha  Amani ambayo kwetu ni fursa kwa  ustawi wa Maendeleo ya kila mmoja wetu na taifa”

Lengo la kuandaa kauli mbiu ya kitaifa ni kutokana na haja ya kuelezea kiini cha migogoro mbalimbali na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini yanayotokana na uwepo wa malalamiko ya migogoro inayoelekea kuvunja na kuhatarisha Amani  ambapo huchangia jamii   kukosa huduma sawa, migogoro ya kisiasa na demokrasia, migogoro ya wakulima na wafugaji hata mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kama taifa tukiweza kijenga umoja na Pamoja Kudumisha Amani, Heshima, Usalama na Utu kwa wote itakaopelekea kuwepo kwa amani ya kudumu kwa jamii nzima, Kwa mf. Tunapo sema Pamoja ni maana pana  sana yaana  yaani kla mmoja wetu bila kujali Ragi, Dini, Itikadi na hata kabila tuungane  na kuwa kitu kimoja ili kudumisha Amani kwa kujenga misingi ya kueshimiana na kuthaminiana utu wetu ili kuimalisha Usalama wetu.

Naomba kutoa wito kwa  Serikali, wanasiasa  wote, Viongozi wa dini, Asasi za Kiraia na jamii zima kuienzi kauli mbui ya mwaka huu ambayo naona inaendana na haja na wto wa kufikia kuwa serikali ya Viwanda, nasema haya kwakuwa Amani ni fursa kwetu kufanya shughuli za Maendeleo kwa uhuru na Amani huku upendo maina ya mtu na mtu ukiaswa kuongezeka badala ya kujengeana chuki sisizo za msingi

Nawaasa watanzania wasiweke udini, itikadi  na ukabila kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha amani iliyopo kupote, hakuna kitu kikubwa na kilicho bora kama amani tupo hapa kwa vile kuna amani tunaabudu kwa ajili ya amani kuna watu wanakuwa wakimbizi ndani ya nchi yao kutokana na kukosa Amani. #Amaninifursa kwa Maendeleo ya Viwanda Tanzania#

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE