September 11, 2017

RISE CHARITY: CHANGIA VIFAA WEZESHI VYA ELIMU KUKUZA TAALUMA NCHINI POKEA CODES TAFADHALIRise Media Group inaendesha kampeni ya Rise Charity yenye lengo la kuwasaidia watoto mbalimbali wa shule zilizo katika mazingira magumu hususani shule za vijijini  vifaa wezeshi katika masomo kama vile Madaftari, Kalamu za wino , Kalamu za risasi, Vitabu nk.

Akizungumzia kampeni hiyo Afisa Habari wa Rise Media Bakari Ngamba amesema kuwa kampeni hiyo imebebwa na kauli mbiu isemayo mtoto kwanza Elimu ni msingi.

“kampeni hii inamakusudio makuu mawili, moja ikiwa ni kuwasaidia watoto wa shule za Msingi waishio vijijini vifaa mbalimbali vya kujifunzia ,Pili ni kuhamasisha watoto kupenda shule na kuwafundisha baadhi ya masomo ya jamii ili waweze kutimiza ndoto zao, Kampeni hii inatarajiwa kuzunguka mikoa mbalimbali Tanzania ”  alisema Ngamba.

Aidha Ngamba amewakaribisha wadau Mbalimbali  wa elimu nchini na nje ya nchi kuungana na Rise Media kwa kuchangia kampeni hii ili kuendeleza elimu nchini pamoja na kudumisha elimu kwa wanafunzi katika kuendeleza na kujenga  Tanzania ya viwanda kwa kumfunza Mtoto kuwa na uzalendo wa kujenga nchi yake kwa kusaidia wengine pindi atakavyo kuwa mkubwa kwani hii ni moja ya kumbu kumbu katika maisha yake.

Vile vile Rise charity ina dhumuni la kuhamasisha mahusiano mazuri baina ya wazazi na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mtoto anapata mahitaji muhimu ya kitaaluma kwa wakati uliokusudiwa.

Akieleza Namna unavyoweza kushiriki katika kuchangia kampeni hiyo  ni kwa kuwasiliana na Mwenyekiti  wa kampeni Ndugu Elia Joseph kwa namba 0716 23 69 12  na Atley Timothy 0719 92 15 64
 

Bakari Ngamba Human Resource Rise Media Company Professional journalist & Mass-Com P.O.BOX 75261, Mob: +255 766 866273 /+255 657 185504, Email: bakaringamba@yahoo.com Blog: http://tanzanianewstza.blogspot.com/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE