September 28, 2017

RC MASENZA ALIOMBA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA KUSHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA UTALII YA KARIBU KUSINI


Image result for amina masenza
Mkuu wa Mkao wa Iringa Amina Masenza (RC) amewaomba washiriki wa baraza la biashara la mkoa kushiriki kikamilifu kwenye maonesho ya Utalii ya karibu Kusini yanayoendelea katika viwanja vya Kichanagni mjini Iringa.
RC alisema ya hayo juzi wakati wa kikao cha baraza la biashara la mkoa wa Iringa kilichofanyika juzi katika ukumbi wa valentine, kihesa-kilolo mjini Iringa.
Masenza alisema kuwa lengo ni kuufanya mkoa wa Iringa kuwa mfano katika ukanda huo wa kusini katika sekta ya utalii.
Zaidi ya wajasiriamali 350 wamejitokeza kushiriki maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayoanza rasmi jana, ambayo yatafunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu hapo tarehe 29.09.2017  hadi Oktoba 2 katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa.
Maonesho hayo yameandaliwa na mikoa ya nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii,  shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido) na wadau mbalimbali ukiwemo Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST).
Alisema kuwa kuna fursa nyingi katika mkoa wa Iringa zinazoanzia katika uwekezaji kwenye sekta ya za utalii ambapo tarehe 29.09.2017 maonesho rasmi ya utalii yatazinduliwa.
“Eneo jingine ni viwanda, biashara, kilimo (maua na matunda), ufugaji, misitu na huduma za kijamii,” alisema.
Aidha, mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mkoa wa iringa umefungua milango na kuowamba wa wakezaji wa ndani na nje kuja kuwakeza baada ya kuweka mazingira wezeshi.
Alisema kuwa wapo wawekezaji wa ndani na nje ambao wamekwisha ziona fursa za uwekazaji zilipo katika mkoa wa iringa na kuzichangamkia.
“Nitoe rai kwa wawekazaji wengine kuzitumia fursa zilizopo. Sisi kama serikali tumejipanga kuwasaidia wawekazaji kutimiza nia yao ya uwekezaji” alisema masenza.
Halmashauri zote katika mkoa wa iringa zimejipanga vema kuwasaidia wawekazji kila wanapojitokeza, aliongezea mkuu wa mkoa huyo.
Awali, mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu alisema kuwa kikao cha baraza la biashara la mkoa ni kikao halali kwa mujinbu wa sheria.
Alisema kuwa kikao hicho kinaundwa na wajumbe kutoka sekta ya umma na binafsi kutoka katika mkoa wa Iringa.
Mwakabungu aliwataka wajumbe kutumia fursa katika baraza hilo ndipo vikwanzo na kero zinazokwamisha maendeleo ya viwanda, kilimo na biashara katika mkoa vitatafutiwa ufumbuzi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE