September 23, 2017

RC MAKALA AOMBWA KUNUSURU UJENZI WA SHULE KIJIJI CHA IJUMBI...

MKUU wa Mkoa Mbeya Amos Makala aombwa kunusuru ujenzi wa shule kuendelea anatupasha mwandishi Ezekiel Kaman mtukiodaimablog ,Mbeya

Wakizungumza na matukiodaimablog wananchi jana wamesema kuwa wamelazimika kutoa ombi hilo kutokana na baada ya   kuenguliwa uongozi Mugabe Sumuni  Mwenyekiti wa Kijiji cha Ijumbi Kata Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya na kumepelekea  ujenzi wa shule shikizi ya Ishungu kumesimama  .

Hali hiyo imekuja baada ya wananchi kutokuwa na imani na uongozi wa Kijiji kwa madai ya  tuhuma za ubadhilifu walionao baadhi yao .

Hivi karibuni Wajumbe wa Serikali ya Kijiji walijaribu kufanya kikao na Kamati ya shule shikizi lakini kikao kilivunjika kutokana na kutofikiwa muafaka wa nini madhununi ya kikao hicho ambapo Wajumbe wa shule walilazimishwa kusaini mahudhurio bila kujua agenda za kikao hali iliyomfanya mtendaji wa Kijiji Julius Mwagala na Wajumbe wa Kijiji kuamua kuondoka.

Baadhi ya wazee wamemuomba Mkuu wa Mkoa  wa Mbeya Amos Makalla kuingilia kati suala hilo haraka vinginevyo wamesema watakwenda Dodoma kumuona Waziri Mkuu kwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Mfune ameshindwa kulipatia ufumbuzi licha ya kuwasilisha vielelezo vya  tuhuma za ubadhilifu vikiwemo stakabadhi na nyaraka mbalimbali.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ruiwa Kassim Abdilah Mtale amesema kama hatua za haraka hazitachukuliwa haraka kabla ya msimu wa mvua kuanza kuna hatari ya watoto zaidi ya mia nne kukosa masomo kutokana na kushindwa kuvuka mto kwenda shule jirani.

 Kijiji cha Ijumbi ndicho Kijiji pekee ambacho hakina shule wala Zahanati kutokana na mvutano wa maslahi binafsi na siasa huko viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wakitoa maamuzi yanayowakanganya wananchi na baadhi watumia mgogoro huo kujinufaisha.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE