September 14, 2017

RATIBA: MECHI ZA VPL WIKIENDI HII ,MASAWE BWILE ANA KWA ANA NA CLEMENT SANGA WA LIPULI FC IRINGA


Mzunguko wa Tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa ratiba ya VPL,  kesho Ijumaa Septemba 15, 2017 Azam FC itaialika Kagera Sugar saa 1.00 usiku (19h00) katika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi jijini Dar es salaam.

Kwa siku ya Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na  Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni (16h00) katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Mbao itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao pia utapigwa Jumamosi saa 16h00 wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine.

Lipuli Fc itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting saa 16h00 katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United saa 16h00 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 Mbeya City itaikaribisha Njombe Mji saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba SC ikiwa mwenyeji wa Mwadui FC saa 16h00 jioni katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE