September 1, 2017

RAIS DKT MAGUFULI ANAFANYA KAZI NZURI AOMBEWE - SHEKHE CHALAMILA

Shekh  wa  mkoa  wa Iringa Abubakari Chalamila

 Waumini  wa   dini ya  kiislam  Arif  Abri kushoto  akisalimia na  mwenzake uwanja  wa  Samora (picha ya  maktaba ya matukiodaima)
.......................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog

SHEKH   wa mkoa wa Iringa, Abubakar Chalamila amesema jitihada  zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli katika   kuliongoza Taifa  ni kubwa hivyo  anapaswa  kuendelea  kuombewa  kila  wakati.

Akitoa  salam za Eid  mara baada ya  sala ya  Eid iliyofanyika katika  uwanja  wa  Samora  mjini  Iringa ,sheikh  Chalamila amesema kuwa   utendaji kazi wa  serikali ya  awamu ya tano  chini ya Rais Dkt Magufuli unaonekana kwa  wananchi  wote wa Taifa  hili  pamoja na nchi nyingine za Afrika na Dunia  hivyo  ili  kuendeleza kazi ya kuliongoza Taifa  vizuri  kila mmoja anapaswa kutenga  muda  wake kwa ajili ya kumuombea Rais .

 Sheikh  Chalamila  amesema  kwa  kuwa  hali ya  uchimi  imeanza  kuonekana jinsi  inavyoimarika  ni  vema watanzania   kuwa na subira  na kuacha kulalamika  kuwa hawana  kitu  mfukoni  ila baada ya kazi ya  kujenga  uchumi  kukamilika watanzania  wote  watafurahia matunda ya Taifa bila  kukitazama kikundi  kidogo cha   watu ambao  walikuwa  wakikumbatia  uchumi wa Taifa .

Akizungumzia  suala la  ulinzi na usalama amesema  kuwa hali ya ulinzi kwa  sasa  imezidi  kuwa  nzuri kwani ndani ya  mkoa wa Iringa hakujawa na matukio yoyote makubwa ya unyang'anyi wa   kutumia  sialaha  zaidi ya matukio ya  vibaka  wa kawaida  na  kuwa kuna uwezekano mkubwa wa  kukomesha matukio hayo  iwapo  jamii itashirikiana na jeshi la  polisi .

waumini  wa dini  ya  kiislam mkoa  wa  Iringa  wakishiriki  kuchinja ng'ombe leo
Sehemu ya  nyama  iliyochinjwa  ikisubiri  kutolewa  msaada  wa wananchi  wenye uhitaji
Zoezi la  uchinjaji wa  ng'ombe ukiendelea  mjini  Iringa leo

Wakati   huo  huo taasisi ya kiislam mkoa  wa Iringa ya  Dhi Nureyn imetumia  kiasi cha  shilingi  milioni 20  kununua ng'ombe 13 na  mbuzi 90 kwa ajili ya kuwapa msaada  watu  wasio na uwezo kwa  ajili ya  kusherekea  sikukuu  hiyo ya Eid .

Katibu  wa Dhi Nureyn Iringa Shams  Elmi alisema kuwa  fedha  hizo zimetokana na  sadaka  zilizotolewa na  waumini mbali mbali wa  dini  hiyo  kwa ajili ya  kununua  mbuzi na  ng'ombe ili  kuwawezesha  wasio na uwezo wa  kuchinja kupata kushiriki  sikukuu  hiyo kama  wenye uwezo.

Alisema  ng'ombe 13 na  mbuzi 45  zimechinjwa  Iringa wakati mbuzi 45  zimesafirishwa kwa  ajili ya uchinjwaji  kama  huo mkoani Dar es Salaam .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE