September 15, 2017

POLISI YAPIGA MARUFUKU MAOMBI KWAJILI YA LISSU JUMAPILI


 Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limeandaa maombi maalumu kwa ajili ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi Septemba 7 akiwa Dodoma.
Maombi hayo yatafanyika Jumapili ijayo katika viwanja vya TIP, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari viongozi mbalimbali wa dini wamealikwa kwa ajili ya kuongoza maombi hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha - Tanzania Bara, Patrick Ole Sosopi amesema tayari wametoa taarifa polisi na mamlaka nyingine zinazohusika kwa ajili ya kufanikisha jambo hill.
"Tunakwenda kufanya maombi na siyo siasa, sisi tumeratibu tu maombi haya lakini hatutazungunza chochote, tutawaacha viongozi wa dini waongoze maombi hayo," amesema kiongozi huyo.

Ole Sosopi amesema wamepeleka barua ya mwaliko kwa taasisi mbalimbali za dini ikiwamo Bakwata, TEC na CCT, hata hivyo amesema bado wanasubiri kujibiwa barua zao.
"Tumetoa taarifa pia kwa jeshi la polisi kama sheria inavyoyaka, hatutarajii kuzuiwa kwa sababu tumefuata taratibu zote kama sheria inavyotaka. Mmiliki wa uwanja amekubali, serikali ya mtaa pia imeridhia jambo hilo," amesema Ole Sosopi na kusisitiza kwamba hili jambo ni la kitaifa na watalifanya kwa amani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE