September 26, 2017

NMB YAWANOA WANACHAMA WA NMB BUSINESS CLUB IRINGA


Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Iringa Odila Ngamilaga akifungua warsha ya wanacha wa NMB business Club mjini Iringa 


BANK ya NMB kwa kupitia tawi lake la NMB Mkwawa Mkoa wa Iringa imeandaa hafla na kuwakusanya wateja wake wadogo na wakati ambao ni wanachama wa klabu ya biashara ijulikanayo kama “NMB Business Club”

ili waweze kuzungumza nao katika ufanikishaji wa biashara zao lakini pia kutoa mafunzo ya kibishara.

Hafla hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa Wafanya biashara mkoa wa Iringa- Bwana Odilo Ngamilaga, Hafla hii  ilifanyika jana na kuhudhuriwa na wafanyibiashara zaidi ya 200 wa Katika Mkoa wa Iringa.
Kusudi kubwa la hafla hii ni kutaka kusikia kutoka kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa na mahitaji waliyokuwa nayo lakini pia kuwapa semina elekezi ili kufikia malengo ya bishara zao.

Ingawa Benki ya NMB imekua na utamaduni wa kukutatana na wateja wake wa Nyanja tofauti tofauti katika nyakati tofauti ili kuwaelezea maendeleo na huduma mbali mbali ambazo NMB inakua imezifikia kwa kusudi la kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wake.

Sisi kama NMB tunayofuraha kubwa sana na tunajivunia  kuwa na wateja wetu leo na tunaamini kwa kupitia mkutano huu na mafunzo ambayo leo mmeyapata yatakuwa mwongozo kila mnapofikiria kukua kibishara zaidi sana nawasihii mzingatie yale yote yaliyotolewa na watoa maada lakini zaidi mzingatie wosia wa mgeni rasmi  amabae pia ni Mfanaya biashara mwenzenu- Mwenyekiti wa wafanyabiasha
ara mkoa wa Iringa Bwana  Odilo Ngamilaga.

"naamini mkiwa na nidhamu katika matumizi ya fedha hasa mikopo ambayo mnayochukua mtafika mbali kibiashara"

Alisema Meneja Mwanandamizi wa uhusiano  kutoka kitengo cha biashara NMB- Wogofya Mfaramagoha.
Nae mgeni rasmi katika hafla hii ,Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Iringa Bwana  Odilo Ngamilaga. Aliwasihi sana wafanya biashara hao kua na nidhamu ya Mikopo inayochukuliwa   .

Alisema wengi wa wafanya biashara hupotoka mara wanapopata mitaji ya bishara zao hudhani kua pesa itabakia katika mikono yao siku zote.Aidha aliupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kuona haja ya kuwa na klabu ya biashara ambayo kusudi lake ni kuwa karibu na wateja wao ili kuhakikisha wanafikia malengo ya biashara zao.

“Kwanza kabisa ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa benki ya NMB nkwa kuona umuhimu wa kuwa na klabu ya biashara hapa Mjini Unguja .

Klabu hiii iwe chachu ya maendeleo kwenu wafanyabishara wa Iringa  ili kusudi hata wale ambao wamekua waoga wa mikopo na waoga wa kufanya biashara wapate ujasiri kutoka kwenu.Lakini pia nitoe angalizo kwenu wafanya biashara , Msibweteke na pesa mnazozipata msidhani pesa hizo zitakaa mikononi mwenu siku zote.

Mnatakiwa kuwa na nidham katika matumizi yenu ya Pesa Mafunzo mnayopewa yakawafae ili muweze kufikia malengo ya Biashara zenu”. Alisema Bwana Ngamilaga. 

Benki ya NMB imfanikiwa kuzindua  klabu za bishara (Business Clubs) katika mikoa yote nchini. Ili kuhakikisha kuwa wanakua karibu na wateja wake NMB imekua ikifanya mikutano na wanachama wa klabu hizi kila mwaka ili kusikia changamoto amabazo wanakutana nazo

.Lakini pia kuwaelezea wateja wao uboreshwaji wa huduma mbali mbali za kibenki  ambao NMB umefanya.NMB wanatoa wito kwa wateja wao kutokua waoga wa kufanya biashara na kuchukua mikopo Benki. “Benki ndie rafiki wa karibu wa mfanya biashara yeyote “ NMB wanase

mmoja kati ya washiriki wa warsha hiyo Happy Mangula alisema kuwa mbali ya kutojiunga na clabu hiyo ila anataraji kujiunga ili kuweza kunufaika zaidi na NMB.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE