September 22, 2017

MWANAFUNZI AKAMATWA AKITAKA KUUZA BUNDUKI


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imemtia mbaroni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Robson Maji (21)kwa kosa la kukutwa akitaka kuuza bunduki aina ya Bastola yenye risasi,
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa akiwa kwenye mipango ya kuuza Bastola aina ya Beretta yenye namba DAA316502 ikiwa na risasi sita.
Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo lilipata taarifa ya kuwepo kwa biashara ya kukodishwa kwa silaha kwa majambazi ili wakafanyie kazi za kiuhalifu na kulipwa fedha na kwamba uliandaliwa mtego maeneo ya TRA Mwenge na kumkamata mtuhumiwa akitaka kukodisha kwa Sh.. 400,000.
Mtuhumiwa huyo aligunduliwa kuwa yupo tayari kuiuza kwa Sh. 2,500,000 na kwamba alipohojiwa alikiri kuiba silaha hiyo kwa Baba yake aitwaye Isaack Maji (51) mkazi wa Tabata Segerea.
Mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alitaja mshirika wake ambaye ni rafiki yake mwanafunzi wa Chuo cha Columbus Staste Cummunity cha nchini Marekani.
Amesema upelelezi unaendelea ili kujua mmiliki halali wa silaha hiyo na mahojiano zaidi yanafanyika ili kuweza kubaini silaha hiyo imekodishwa mara ngapi na imetumika na watu gani

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE