September 3, 2017

MWALIMU MKUU MATATANI KWA TUHUMA ZA MAUWAJI YA MWANAFUNZI WAKE KWA FIMBO

RC Iringa Amina Masenza 
.....................................................................
    Na  MatukiodaimaBlog
JESHI  la  polisi  mkoa  wa  Iringa linamshikilia mwalimu  mkuu  wa  shule ya  msingi Ng'angula   Robson Sanga (59)  kwa  tuhuma za  kumua mwanafunzi  wake  wa  darasa la tano Emmanuel Canal Gavile (13) kwa  kumchapa fimbo mapajani  kwa  kosa la  uchelewaji  shule .
Imeelezwa  kuwa  mwalimu  huyo  alichukua  uamuzi  huo wa  kumwadhibu  kwa fimbo  mwanafunzi  huo baada ya  kuchelewa namba asubuhi  shuleni hapo  na  hivyo adhabu ambayo aliamua  kuitumia  kumwadabisha  mwanafunzi  huyo ni  kumpa dozi kali ya viboko hadi  mwanafunzi  huyo  alizidiwa.
Akizungumzia  tukio hilo kamanda wa  polisi wa  mkoa wa Iringa  jana Julius Mjengi alisema kuwa  tukio  hilo  lilitokea Agosti 16 majira ya saa 3 asubuhi mwaka  huu katika  shule ya msingi  Ng'ingula  wilaya ya  Kilolo mkoani hapa  kosa  la  kuchapwa  kwa  mwanafunzi huyo likiwa ni uchelewaji  shule .
Alisema  kufuatia  adhabu hiyo  mwanafunzi huyo  alianza kulia maumivu kiasi cha  kushindwa kujisomea na  wenzake na  hivyo  kulazimika  kukimbizwa  Zahanati ya  kijiji  hicho ambako hali  ilizidi  kuwa mbaya na  kuhamishiwa  kituo cha  afya  Usokomi wilaya ya  Kilolo.
" Agosti  26 mwaka  huu  mwanafunzi  huyo  alihamishiwa katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa akilalamikia  maumivu makali katika paja  lake la mguu wa  kulia kabla ya  kufariki  dunia  majira  ya  saa 3 asubuhi "
Alisema  kuwa  uchunguzi  wa daktari  umeonyesha  kuwa  kifo  cha mwanafunzi  huyo kilisababishwa na mpasuko wa mfupa  wa paja la mguu  wa kulia pamoja damu kuviria katika  mapafu yake .
Kamanda Mjengi  alisema kwa  muda  wote  huo  wazazi  hawakuweza  kuripoti polisi  ila  baada ya kifo cha mwanafunzi  huyo ndipo  walipofika  kituo  cha polisi kutoa taarifa na  jeshi la polisi lilifanikiwa  kumkamata  mwalimu  huyo siku  hiyo hiyo.

Kamanda Mjengi  alisema kwa  muda  wote  huo  wazazi  hawakuweza  kuripoti polisi  ila  baada ya kifo cha mwanafunzi  huyo ndipo  walipofika  kituo  cha polisi kutoa taarifa na  jeshi la polisi lilifanikiwa  kumkamata  mwalimu  huyo siku  hiyo hiyo na  uchunzi  wa jeshi la  polisi  unaendelea  juu ya  tukio  hilo kabla ya mwalimu  huyo  kufikishwa mahakamani kwa  tuhuma  za mauwaji .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE