September 25, 2017

MWAKYEMBE: SIJAFUTA MASHINDANO YA MISS TANZANIA NA TUZO ZA MUZIKI

Mwakyembe+picha
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Dk Harisson Mwakyembe amesema hajayafuta mashindano ya Miss Tanzania na Tuzo za muziki ila kilichopo ni kwamba Mashindano hayo Yanaanzishwa na kujifuta yenyewe kutokana na kushindwa kufanyika kwa wakati na mwendelezo kwa sababu mbalimbali za waandaaji kushindwa kuyaandaa mashindano hayo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo kwa njia ya Simu wakati akizungumza na Fullshangwe iliyotaka kupata ufafanuzi kuhusiana na  uvumi uliokuwa ukisambaa  kwenye mitandao ya kijamii kwamba amefuta mashindano hayo na tuzo za muziki.
Ameongeza kwamba ameelekeza Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza kuliangalia suala hilo na kulitolea ufafanuzi kulingana na changamoto zilizopo kwani ni muhimu tukawa na Tuzo na mashindano yenye Muendelezo, Tija na yenye kutoa zawadi kwa washindi kadiri zawadi hizo zilivyopangwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE