September 8, 2017

MECHI YA SIMBA VS AZAM YARUDISHWA SAA 10:00 JIONI KWA SABABU ZA KIUSALAMAMCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Azam FC na Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, umerudishwa saa 10:00 jioni kutoka saa 1:00 usiku.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama, baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kusema kwamba ni hatari mechi hiyo kuchezwa usiku na imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuirudisha saa 10:00 jioni.

Mambo mengine yote yanabaki kama yalivyopangwa na mchezo huo utachezeshwa na refa Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani na mezani atakuwepo Josephat Bulali na Kamisaa  atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es Salaam, wakati viingilio ni Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP na 7,000 kwa mzunguko.

Timu zote zilianza kwa ushindi katika mechi zao za kwanza Ligi Kuu, Azam FC wakishinda 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara huku Simba wakishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Na kesho makocha wa timu zote, Mcameroon Joseph Marius Omog, na Mromania Aristica Cioaba, watataka kuendeleza wimbi la ushindi katika jitihada za kuipokonya taji Yanga SC.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE